Coming Up Tue 6:00 PM  AEDT
Coming Up Live in 
Live
Swahili radio

Australia yazindua COVIDSafe; programu ya mawasiliano ya ufuatiliaji maambukizi virusi vya corona

A close up of the government's coronavirus tracing app. Source: SBS

Australia yazindua COVIDSafe; programu ya serikali kusaidia kuwasiliana na watu waliombukizwa virusi vya COVID -19. Ni programu ya simu ya mkononi na hapa ni kipi unachohitaji kujua.

Programu imeundwa kwa nini?

Programu inatarajiwa kuboresha utafutaji wa kesi za virusi vya corona na watu walioakumbana nao. Itawezesha utambulisho wa watu ambao wanaweza kuwa wamekutana na mwenye virusi, kupitia data iliyohifadhiwa kwenye simu, mara moja itakapopatikana kwa mamlaka ya afya.

Mawasiliano yatarekodiwa ikiwa mtu yuko ndani ya umbali wa m 1.5 ya mtu mwingine huku programu imefunguliwa na mawasiliano hayo kukaa kwa angalau dakika 15.

Kujiandikisha kwa programu ya COVIDSafe ni kwa hiari. Serikali inapendekeza wakaazi wote wa Australia kuipakua kwa sababu Waaustralia zaidi wanapounganisha kwenye programu ya COVIDSafe, itakuwa wepesi zaidi kuweza kufuatilia hali ya virusi.

Je! Watendaji watatumiaje data za COVIDSafe?

Programu ya COVIDSafe iliundwa kuharakisha mchakato wa mwongozo wa sasa wa kupata watu ambao wamekutana kwa karibu na mtu aliye na COVID-19. Utaratibu huu unapaswa kupunguza nafasi za kupitisha virusi kwa familia, marafiki na watu wengine katika jamii, bila kufahamu.

Maafisa wa afya wa majimbo na vitongoji wanaweza tu kupata taarifa za programu ikiwa mtu atatambulika ana virusi na akikubali taarifa iliyoko kwenye simu yake kupakuliwa. Maafisa wa afya wanaweza kutumia tu taarifa za programu kusaidia kuonya wale ambao wanaweza kuhitaji kuweka karantini au kupimwa.

Programu ya COVIDSafe ndio programu ya mawasiliano pekee iliyoidhinishwa na serikali ya Australia. Kwa taarifa zaidi, tembelea tovuti ya COVIDSafe app Health Department.

Je! Unashiriki taarifa gani ya kibinafsi kupitia programu ya COVIDSafe?

Watumiaji wanapopakua programu, wanapeana jina lao, nambari ya simu ya mkononi, na nambari ya posta na kuchagua safu ya umri. Kisha watapokea ujumbe wa maandishi wa uthibitisho wa SMS kukamilisha usakinishaji(installation). Kisha mfumo huunda nambari maalum ya kumbukumbu iliyosimbwa(encrypted).

COVIDSafe inatambua vifaa vingine na programu ya COVIDSafe iliyosanikishwa(installed) na Bluetooth iliyowezeshwa. Wakati programu inatambua mtumiaji mwingine, inabaini tarehe, saa, umbali na muda wa mawasiliano na nambari ya kumbukumbu ya mtumiaji mwingine. Programu ya COVIDSafe haifai kukusanya eneo la watumiaji.

Serikali ya Australia inasema kwamba taarifa hiyo imesimbwa(encrypted) na kwamba kitambulisho kilichosimbwa huhifadhiwa salama kwenye simu ya mtumiaji. Taarifa ya mawasiliano iliyohifadhiwa kwenye simu za mkononi za watu zitafutwa kwenye mzunguko baada ya siku 21. Kipindi hiki kinazingatia kipindi cha kuangilia hali ya virusi vya COVID-19 na wakati unaochukua kwa kupimwa.

Ni nini hufanyika wakati mtumiaji wa programu anapatikana na maambukizi?

Mtu anapogundulika na COVID-19, taarifa za mawasiliano iliyosimbwa(encrypted) kutoka kwa programu itapakiwa kwenye mfumo salama wa uhifadhi wa taarifa, ikiwa mtumiaji atatoa ruhusa. Maafisa wa afya wa majimbo na vitongoji basi wata:

  • tumia anwani zilizokamatwa na programu ili kusaidia ufuatiliaji wao wa kawaida wa mawasiliano
  • piga simu kwa watu kuwafahamisha wao au wazazi wao / walezi wao wajue wanaweza kuwa wamepata maambukizi.
  • toa ushauri juu ya hatua zifuatazo, pamoja na:
  • cha kutafuta nje
  • lini, vipi na wapi watapimwa
  • nini cha kufanya kulinda marafiki na familia kutoka kwa maambukizi
  • Maafisa wa afya hawatamtaja mtu aliyeambukizwa.

Ikiwa unajali juu ya usiri wa data zako, soma Sera za faragha.

Watu nchini Australia lazima wakae umbali wa mita 1.5 kutoka kwa wengine na mikusanyiko ni mdogo kwa watu wawili isipokuwa ukiwa na familia yako au mkazi wa kaya moja.

Ikiwa unaamini unaweza kuwa umeambukizwa virusi, piga simu kwa daktari wako (usitembelee) au wasiliana na Simu ya kitaifa ya Habari ya Afya ya Virusi vya Corona kwa simu namba 1800 020 080. Ikiwa unasumbuka kupumua au unahitaji dharura ya matibabu, piga simu 000.

SBS imejitolea kuarifu jamii tofauti za Australia kuhusu maendeleo ya hivi karibuni ya COVID-19. Habari na taarifa zinapatikana katika lugha 63 kupitia sbs.com.au/coronavirus.

Source SBS News, Australian Government Department of Health