Coming Up Sun 10:00 PM  AEST
Coming Up Live in 
Live
Swahili radio

Kipi ni lazima kujua kuhusu Covid-19 kupitia lugha yako

SBS imejitolea kutoa taarifa za kuaminika ambazo zinakufanya uwe na habari juu ya mlipuko wa COVID-19 - kwa lugha yako. Kipeperushi cha maelezo muhimu kinajumuisha taarifa za lazima kuzielewa kwa kila mtu katika jamii.

Kaa nyumbani. Kaa salama. Endelea kushikamana. Okoa maisha.

Kwa taarifa zaidi za SBS COVID-19 jimbo kwa jimbo, BONYEZA HAPA 

Matatizo ya kifedha

"Ikiwa unakumbana na matatizo ya kifedha tembelea www.moneysmart.gov.au au piga simu Msaada wa Madeni Kitaifa kwa namba 1800007007.

Malipo ya watafuta kazi na utunzaji ajira (Jobseeker na Jobkeeper) 

Malipo ya wenye mikataba ya ajira za kudumu (JobKeeper) yataendelea hadi mwezi Machi 2021, na malipo ya watafutaji kazi (JobSeeker) hadi mwezi Desemba 2020. Katika miezi michache ijayo, serikali itatangaza mpango wa watafutaji kazi (JobSeeker.

Malipo yatapunguzwa kuanzia mwezi Septemba 2020.

Malipo ya kazi (Jobseeker)

-Sasa: $1,115

-Kuanzia Septemba 2020: $815

Pia, kuanzia mwisho wa Septemba, unaweza sasa kupata $300 kwa wiki mbili badala ya $106, kabla ya malipo yako ya Jobseeker hayajaathiriwa.

Kuanzia Agosti 4 yoyote anayepokea malipo ya ukosefu wa ajira lazima ajiunge na huduma za kutafuta ajira na atafute kazi nne kwa mwezi, ili aendelee kupokea malipo.

Utunzaji ajira (Jobkeeper)

Yamegawanywa katika sehemu mbili, moja kwa wale wenye mikataba ya ajira za kudumu, na nyingine kwa wenye mikataba mifupi.

Malipo ya wiki mbili kwa wafanyakazi wenye mikataba ya kudumu:

-Sasa: $1,500

-Kuanzia Septemba 2020: $1,200

-Kuanzia Januari 2021: $1,000

Malipo ya wafanyakazi wa mikataba mifupi:

-Sasa: $1,500

-Kuanzia Septemba 2020: $750

Kuanzia January 2021: $650

 

Jinsi gani COVID-19 inaenea?

COVID-19 inaenea kutoka kwa mtu hadi kwa mtu kupitia:

 • Kuwasiliana kwa karibu na mtu wakati anaambukiza au katika masaa 24 kabla ya dalili zao kuonekana.
 • Kukaa karibu sana na mtu aliye na maambukizi aliyethibitishwa ambaye hukohoa au kupiga chafya.
 • Kugusa vitu au nyuso (kama vile vipuli vya mlango au meza) vilivyochafuliwa kutokana na makohozi au kupiga chafya kutoka kwa mtu aliye na maambukizi yaliyothibitishwa, kisha kugusa mdomo wako au uso.

Serikali ya Australia inapendekeza kwa wakazi wote kupakua programu ya COVIDSafe. Soma zaidi

Dalili za COVID-19 ni nini?

Dalili za Virusi vya Corona zinaweza kuanzia kutoka ugonjwa mdogo hadi pneumonia, kwa mujibu wa tovuti ya Serikali ya Shirikisho.

Dalili za COVID-19 ni sawa na zile zingine za homa na mafua na ni pamoja na:

 • Homa
 • Kuwashwa kwa koo
 • Kikohozi
 • Uchovu
 • Ugumu wa kupumua
 • Dalili zingine zinaweza jumuisha, kutokwa na makamasi, kichwa kuuma, maumivu ya misuli au viungo, kichefuchefu, kuharisha, kutapika, kukosa uwezo wa kutambua harufu, mabadiliko ya kutambua ladha, kukosa hamu ya kula na uchovu.

Mamlaka imetengeneza mfumo wa kuangalia Dalili za COVID19 ambao unaweza kuutumia ukiwa nyumbani: https://www.healthdirect.gov.au/symptom-checker/tool/basic-details

Je! Nifanyeje ikiwa ninaonyesha dalili?

Ikiwa unapata dalili ndani ya siku 14 baada ya kuwasili nchini Australia au kati ya siku 14 za kuwasiliana na mtu ambaye amethibitishwa na COVID-19, unapaswa kupanga kumuona daktari wako kwa tathmini ya haraka.

Mpigie simu daktari wako kupanga wakati au wasiliana na Simu ya kitaifa ya habari ya Afya ya Virusi vya Corona kwa namba 1800 020 080. Usitembelee kliniki ya afya au hospitali bila kuwaambia kuwa una dalili.

Kabla ya kufika, piga simu kliniki ya afya au hospitali na uwaambie historia yako ya kusafiri au kwamba umekuwa na ukaribu na aliyethibitishwa kuwa na COVID-19. Lazima ubaki peke yako nyumbani kwako, hoteli au kwenye eneo la  huduma za afya hadi pale mamlaka ya afya ya umma itakapothibitisha kwamba ni salama kwako kurudi kwenye shughuli zako za kawaida.

Ikiwa unataka kuzungumza na mtu kuhusu dalili zako, piga simu kwa Msaada wa kitaifa wa virusi vya Corona kupata ushauri. Simu yao hufanya kazi masaa 24 kwa siku, siku saba za wiki: 1800 020 080

Serikali ya Australia imeanzisha kliniki za masuala ya upumuaji za GP nchi nzima kuwatibu watu wenye dalili za wastani hadi kali za COVID-19 (homa, kikohozi, upungufu wa pumzi, koo na / au uchovu).

Tafuta ikiwa kuna GP kliniki za matatizo ya upumuaji katika jimbo lako/kitongoji na karibu na eneo lako na jinsi ya kujiandikisha kwa miadi.

Ikiwa bado hakuna kwenye eneo lako, tembelea kituo cha afya au tovuti ya Idara ya afya katika jimbo au kitongoji chako kwa maelezo zaidi juu ya kliniki za magonjwa ya homa na matibabu mengine.

Ikiwa unahangaika kupumua au una dharura ya matibabu, piga simu 000.

 

Je! Ninapaswa kupimwa COVID-19?

Baraza la Mawaziri la Kitaifa la Australia limekubali kupanua vigezo vya upimaji nchini Australia kwa watu wote wenye dalili za wastani za COVID-19 ili kubaini kesi haraka.

Virusi hutibiwaje?

Hakuna matibabu maalumu ya ugonjwa wa virusi vya corona, lakini dalili nyingi zinaweza kutibiwa kwa msaada wa matibabu. Dawa za viuadudu hazifanyi kazi dhidi ya virusi.

Ni nani aliye katika hatari kubwa ya kuumwa sana?

Watu wengine ambao wameambukizwa wanaweza kukosa kuwa wagonjwa, wengine watapata dalili kali ambapo watapata nafuu kirahisi, na wengine wanaweza kuwa wagonjwa sana, kwa haraka sana. Kutoka kwa uzoefu wa zamani na magonjwa mengine, watu walio kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa vibaya ni:

 • Waaborigino na watu wa visiwani Torres Strait, wenye umri zaidi ya miaka 50 na wazee walio na moja au magonjwa zaidi sugu
 • Watu wenye miaka 65 na wazee walio na hali ya magonjwa sugu. Magonjwa hayo yanajumuisha kwa tafsiri ya 'magonjwa sugu' itafafanuliwa kadri ushahidi zaidi unavyoibuka.
 • Watu wenye umri wa miaka 70 na wazee
 • Watu walio na kinga dhaifu

Unawezaje kusaidia kuzuia kuenea kwa COVID-19?

Kuzoea kuweka mikono safi na kupiga chafya vizuri/kukohoa na kujiweka mbali kutoka kwa wengine unapokuwa mgonjwa ni njia bora ya kujilinda dhidi ya virusi vingi. Unapaswa:

 • Usiondoke nyumbani kwako isipokuwa imekulazimu kufanya hivyo
 • Endelea kuzingatia kutokuwa karibu na wengine kwa takribani mita 1.5 na zingatia sheria ya mtu 1 kwa mita za mraba 4.
 • Osha mikono yako mara kwa mara na sabuni na maji, kabla na baada ya kula, na baada ya kwenda choo.
 • Funika kikohozi chako na kupiga chafya, toa tishu, na utumie vitakasa mikono vinavyotokana na pombe.
 • Ikiwa haujiskii vizuri, epuka kukutana na wengine (kaa zaidi ya mita 1.5 kutoka kwa watu).
 • Jizoeshe jukumu la kibinafsi na ukae nyumbani kadri uwezavyo.

Nani anahitaji kujitenga?

1) Watu wote ambao wanawasili Australia kuanzia usiku wa tarehe 15 Machi 2020, au wanaofikiria kuwa walikuwa na ukaribu sana na waliothibitishwa kuwa na COVID-19, wanahitajika kujitenga kwa siku 14.

2) Wasafiri wote wanaofika Australia kutoka usiku wa manane tarehe 28 Machi 2020, watalazimika kujitenga kwa siku 14 katika maeneo yaliyoandaliwa (kwa mfano, hoteli).

Wasafiri watasafirishwa moja kwa moja kwenda kwenye maeneo hayo yaliyotengwa baada ya ukaguzi wa uhamiaji, kitengo cha forodha na ukaguzi wa afya ulioimarishwa.

Wafanyikazi wa ADF wataongeza juhudi za polisi katika kutembelea nyumba na makazi ya Waaustralia ambao wametengwa kwa lazima kama ilivyoelekezwa na serikali za jimbo na vitongoji na wataripoti kwa polisi wa eneo hilo ikiwa mtu huyo anayetambuliwa alikuwa nyumbani.

3) Ikiwa umegunduliwa na COVID-19, lazima ukae nyumbani:

 • usiende kwenye maeneo ya umma kama vile kazini, shuleni, vituo vya ununuzi, chekechea au chuo kikuu
 • muulize mtu akuletee chakula na mahitaji mengine na waviache kwenye mlango wako wa mbele
 • usiruhusu wageni ndani - il tu watu ambao kawaida wanaishi na wewe wanapaswa kuwa nyumbani kwako

Kutengamana na watu

Kutengamana na watu ni njia moja ya kusaidia kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi kama vile COVID-19. Nafasi zaidi kati yako na wengine, ni ngumu zaidi kwa virusi kuenea.

Inajumuisha kujizuia kugusa vitu au maeneo (kama vile vitasa vya mlango au meza) zilizochafuliwa kutokana na kikohozi au kupiga chafya kutoka kwa mtu aliye na kesi iliyothibitishwa ya COVID-19.

Kaa nyumbani

Mwongozo madhubuti wa Baraza la Mawaziri la kitaifa kwa Waaustralia wote ni kukaa nyumbani isipokuwa kama:

 • ununuzi wa kile unahitaji - chakula na vifaa muhimu;
 • mahitaji ya matibabu au kiafya, pamoja na mahitaji ya misaada;
 • jizoeshe kufuata sheria zilizopangwa kwa makutano ya hadhara;
 • fanya kazi na usome ikiwa huwezi kufanya kazi au kujifunza kwa mbali.

Je! Ninaweza kutembelea familia na marafiki katika sehemu za huduma za wazee?

Kama sheria ya jumla kwa Australia yote, usitembelee vituo vya utunzaji wa wazee ikiwa:

 • Umerudi toka nje ya nchi katika siku 14 zilizopita.
 • Ulikuwa na ukaribu na aliyethibitishwa kuwa na virusi vya COVID-19 katika siku 14 zilizopita.
 • Kuwa na homa au dalili za maambukizo ya kifua (kv. Kikohozi, maumivu ya koo, upungufu wa pumzi).
 • Kuanzia tarehe 1 Mei lazima uwe na chanjo yako ya mafua ili kutembelea kituo chochote cha utunzaji wa wazee.

Kumbuka majimbo na vitongoji vina vikwazo maalumu katka himaya zao, ambapo haviwezi ingiliana na mapendekezo ya Baraza Kitaifa.

Je! Napaswa kuvaa vikinga uso vya upasuaji(barakoa)?

Mlipuko wa maambukizi ya COVID-19 hivi karibuni kwenye jumuiya nchini Australia inamaanisha majimbo na vitongoji kwa sasa vinashauri au vinahimiza matumizi ya uvaaji barakoa (masks).

Barakoa kwa sasa zinahitajika au kushauria katika jimbo la Victoria (inategemeana na unapoishi) kwa sababu ya idadi kubwa ya maambukizi katika jumuiya ya virusi vya corona. https://www.dhhs.vic.gov.au/face-coverings-1159pm-wednesday-22-july

Watu katika jimbo la New South Wales wameombwa kuvaa barakoa ikiwa wanatoka majumbani au makazini katika maeneo yenye maambukizi makubwa na kwenye sehemu ambazo ni ngumu kuwa mbali na watu.

Wakati barakoa zinaweza tumika kama tahadhari, lazima uendelee:

 • kukaa nyumbani kama hujisikii vizuri
 • dumisha kukaa mbali na watu (umbali zaidi ya mita 1.5), ukiwa nje.
 • epuka mikusanyiko mikubwa na  na sehemu za ndani zilizo na misongamano.
 • jizoeshe kuosha mikono na kutumia vitakasa

Ikiwa hali itabadilika katika jimbo au kitongoji chako hivyo ushauri wa barakoa unaweza kubadilika. Ni muhimu kupata taarifa mpya za ushauri katika eneo lako. Serikali yako ya jimbo au kitongoji itakupa taarifa hizo kupitia: 

https://www.health.gov.au/news/health-alerts/novel-coronavirus-2019-ncov-health-alert/how-to-protect-yourself-and-others-from-coronavirus-covid-19

Kusafiri kutoka, kuingia au ndani ya Australia

Waaustralia lazima waepuke safari zote zisizo za muhimu za nchini. Majimbo na vitongoji vinaweza kutumia vizuizi vyake, ikijumuishwa kufunga mipaka yao ya jimbo.

Kanuni za Kitaifa za Usafiri wa Umma

Huduma za usafiri wa umma ni jukumu la majimbo na vitongoji, na Baraza la Mawaziri la Kitaifa limeweka kanuni kadhaa za kusaidia kudhibiti afya na usalama wa wafanyakazi na abiria kwenye vyombo vya usafiri wa umma, pamoja na: kutosafiri wakati ukijihisi kuumwa, kuzingatia umbali kutoka kwa madereva na abiria wengine, na epuka kutumia pesa taslimu. Watumiaji wa usafiri wa umma hawahitajiki kuvaa barakoa lakini wanaweza kufanya hivyo kwa hiari. Taarifa zaidi juu ya Misingi ya Operesheni za Usafiri wa Umma za COVID-19 tembelea:https://www.inferals.gov.au/transport/files/COVID19_public_transport_principles_29052020.pdf

Safari za Kimataifa

Wasafiri wote wa kimataifa wanaowasili Australia bila kujali utaifa au sehemu waliyotoka ni lazima wakamilishe kujitenga kwa siku 14 katika vituo vilivyotengwa kabla ya kuelekea makwao.

Watapimwa virusi vya corona wakiwa wanaingia katika kujitenga na kabla hajaruhusiwa kuondoka.

Unaweza pia kulazimika kuchangia gharama ya kuwa karantini. Mahitaji haya yanasimamiwa na kutekelezwa na serikali za majimbo na vitongoji:

NSW: https://www.nsw.gov.au/covid-19/travel-and-transport-advice

VIC: https://www.dhhs.vic.gov.au/information-overseas-travellers-coronavirus-disease-covid-19

ACT: https://www.covid19.act.gov.au/community/travelling-and-transport

NT: https://coronavirus.nt.gov.au/stay-safe/quarantine

QLD:https://www.qld.gov.au/health/conditions/health-alerts/coronavirus-covid-19/protect-yourself-others/quarantine

SA:https://www.covid-19.sa.gov.au/restrictions-and-responsibilities/travel-restrictions

TASMANIA:https://www.coronavirus.tas.gov.au/travellers-and-visitors

WA: https://www.wa.gov.au/organisation/department-of-the-premier-and-cabinet/covid-19-coronavirus-travel-wa

Raia wa Australia na wakazi wa kudumu hawawezi kusafiri nje ya nchi kutokana na vikwazo vya COVID-19.

Walakini, ikiwa unataka kuondoka Australia, unaweza kuomba mtandaoni kusamehewa kwa dharura kusafiri ikiwa utakuwa chini ya moja ya makundi yafuatayo:

 • kusafiri kwako ni kama sehemu ya muitikio wako kwa mlipuko wa COVID-19, pamoja na utoaji wa misaada
 • kusafiri kwako ni muhimu kwa mwenendo wa viwanda muhimu na biashara (pamoja na viwanda vya usafirishaji nje na uagizaji)
 • unasafiri kupata matibabu ya haraka ambayo hayapatikani nchini Australia
 • unasafiri kwa biashara binafsi ya haraka na isiyoweza kuepukika
 • misaada au misingi ya kibinadamu
 • kusafiri kwako ni kwa faida ya kitaifa.

Sehemu za kubadilisha usafiri

Sheria za kusafiri zinabadilika kwa haraka. Ikiwa umeamua kurudi Australia:

 • angalia njia yako kwa uangalifu na uwasiliane na ndege yako au wakala wa kusafiri
 • fuata tangazo rasmi kutoka kwa viwanja vya ndege unavyounganisha usafiri wako na mamlaka zinazohusika
 • wasiliana na ubalozi wa karibu au ofisi ya balozi ndogo ya nchi ambazo unapitia ikiwa una maswali yoyote juu ya mahitaji yao ya kuingia au mahitaji ya kutoka.

Tembelea www.smartraveller.gov.au kwa maelezo zaidi na taarifa mpya.

Je! Viongozi wa Australia wanasimamia vipi mlipuko?

Waziri Mkuu ameanzisha Mpango wa Kukabiliana na Dharura kwa Virusi vya Corona (COVID-19).

Gavana Mkuu wa Australia ameongeza kipindi cha dharura cha huduma za kibinaadamu za kujikinga na mlipuko wa maambukizi kwa miezi mitatu kuanzia tarehe 17 Juni 2020 hadi tarehe 17 Septemba 2020.

Vifungu vya ugumu wa nishati, maji na viwango

Mamlaka hutoa chaguzi rahisi za malipo kwa kaya zote na biashara ndogo ndogo zilizo kwenye matatizo ya kifedha kwa:

 • Kutokukataza kuzuia utoaji/huduma kwa wale walio kwenye matatizo ya kifedha;
 • Kurejelea kesi za urejeshaji wa deni na orodha ya waliokataliwa mikopo;
 • Kusamehe ada za ucheleweshaji marejesho na malipo ya riba kwa deni; na
 • Kupunguza kutokuwakatia huduma kulikopangwa kwa kazi muhimu.
 • Wale ambao wanaweza kuendelea kulipa bili zao wanahitaji kuendelea kufanya hivyo - hii ni muhimu ili kuhakikisha uwezekano wa kuendelea kwa watoa huduma muhimu.

Kubadilika kwa wenye vibali vya kuishi(visa) wingine

Wamiliki wa visa za likizo na kazi: Msamaha kutoka kizuizi cha kazi cha miezi sita kwa mwajiri mmoja, ikiwa wanafanya kazi katika tasnia muhimu: afya, utunzaji wa wazee, utunzaji wa walemavu, utunzaji wa watoto, kilimo na chakula, na atastahili visa zaidi ikiwa visa ya sasa inaisha katika miezi sita ijayo.

Programu za Wafanyakazi wa Msimu na Washiriki wa Mpango wa Wafanyakazi wa Pasifiki: wataweza kuongeza visa zao hadi mwaka mmoja.

Wamiliki wa visa za ujuzi za muda: ikiwa wamepoteza kazi, wana siku 60 za kupata mfadhili mwingine au kuondoka Australia (hata kama wana akiba au msaada wa familia)

Ikiwa wamesimamishwa lakini hawajafukuzwa kazi, au wamepunguziwa masaa yao, haitazingatiwa kuwa ni uvunjaji wa visa zao. Wanaweza kupata hadi $10,000 kwa fedha zao za mafao katika mwaka huu wa fedha.

Wanafunzi wa kimataifa:

Wanaweza kuendelea kukaa ikiwa bado wana kazi. Ikiwa hawana kazi, msaada wa familia au akiba, wanaweza kuhitaji kuzingatia mipango mingine.

Wanafunzi wa kimataifa wanaofanya kazi katika sekta ya huduma za wazee na wauguzi wanaruhusiwa kufanya kazi zaidi ya masaa 20 kwa wiki.

Wanaweza pia kupata idhini ya mafao yao ikiwa wamekuwa nchini Australia kwa angalau miezi 12.

Huko Victoria, wanafunzi wa kimataifa watapata malipo ya unafuu wa hadi $1,100 kama sehemu ya kifurushi cha msaada wa dharura cha Serikali ya Victoria ambayo itasaidia makumi ya maelfu ya watu katika jimbo hilo.

Watalii: warudi katika nchi zao, haswa wale wasio na msaada wa kifamilia.

Huduma za watoto

Karibu familia milioni moja wamepangwa kupata fungu la utunzaji wa watoto bure wakati wa janga la virusi vya corona. Chini ya mpango huo, Serikali italipa asilimia 50 ya mapato ya sekta hiyo hadi kiwango kilichopo cha saa kulingana na hatua kwa wakati kabla wazazi kuanza kuwaondoa watoto wao kwa idadi kubwa.

Msaada wa unyanyasaji wa majumbani

Dola milioni 150 zitatumiwa kusaidia Waaustralia wanaopata unyanyasaji majumbani, kifamilia na kijinsia kwa sababu ya kuzuka kwa ugonjwa.

Msaada wa afya ya akili

Dola milioni 74 za awali zitatumika kusaidia matatizo ya afya ya akili na ustawi wa Waaustralia wote. Jalada la kidigitali la serikali la masuala ya afya ya akili linalojulikana kama Head to Health (www.headtohealth.gov.au), litakuwa chanzo kimoja cha habari na mamlaka ya mwongozo wa jinsi ya kudumisha afya njema ya akili wakati wa janga la virusi vya corona na kujitenga, jinsi ya kusaidia watoto na wapendwa wako, na jinsi ya kupata huduma zaidi za afya ya akili na utunzaji.

 

 

 • Watu nchini Australia lazima wakae umbali wa mita 1.5 kutoka kwa mwingine. Angalia vizuizi vya makutano katika jimbo lako. https://www.sbs.com.au/language/english/how-australia-s-states-and-territories-are-relaxing-coronavirus-restrictions
 • Ikiwa unajihisi na dalili za homa au mafua, kaa nyumbani na panga hatua za upimaji kwa kumpigia daktari wako au kuwasiliana na namba ya watoa huduma za maelezo ya afya kitengo cha virusi vya corona kupitia 1800 020 080.
 • Habari na maelezo yanapatikana kwa lugha 63 kupitia sbs.com.au/coronavirus