Coming Up Sun 10:00 PM  AEDT
Coming Up Live in 
Live
Swahili radio

Mwongozo wa Makazi: Jinsi yakutambua mshtuko wa moyo

Mshtuko wa moyo Source: Pixabay

Je wajua dalili za onyo la mshtuko wa moyo?

Afya nzuri maishani hupunguza uwezekano wa mshtuko wa moyo ila, ikitokea unastahili kumbuka dalili na uchukua hatua haraka.

Nini hutokea mtu anapo kumbwa kwa mshtuko wa moyo?

Heart
Pixabay

“Moja ya mishipa inayo safirisha hewa safi na damu moyoni inapo ziba, moyo hauwezi pona chini ya mazingira hayo", mtaalam wa moyo Garry Jennings kutoka shirika la Australian Heart Foundation alieleza SBS Radio.

Umeshauriwa umwone daktari wako, akufanyie unchuguzi wa afya ya moyo wako, nakutathmini athari yako, haswa kama una historia ya mishtuko ya moyo katika familia yako.

Je kuna aina gani za athari?

Shinikizo la damu

Ni wakati shinikizo la damu yako iko juu, moyo wako na mishipa inaweza lemewa. Ila inaweza tibiwa, kwa hiyo mwone daktari wako mara kwa mara ili achunguze shiniko la damu yaku.

Blood pressure - AAP
Anthony Devlin/PA Wire

Kiwango cha juu cha mafuta

Jaribu kuepuka matumizi ya mafuta mengi ndani ya chakula chako. Ukosefu wa usawa wa mafuta ndani ya damu yako inaweza sababisha mshtuko wa moyo au kiharusi.

Chakula kibaya na kisukari

Vegetables and fruits
Vegetables and fruits
GettyImages/fcafotodigital

Chakula kibaya kina weza sababisha unene, ambao huongeza athari ya mshtuko wa moyo na matatizo mengine ya afya. Unapo tumia chakula chenye usawa na afya nzuri unaweza punguza unene, shinikizo la damu na mafuta mwilini.

Shirika la Diabetes Australia nalo lime toa mapendekezo ya jinsi yaku kabiliana na kisukari chako, kusaidia kuepuka msthuko wa moyo.

Uhaba wa mazoezi ya mwili

Kutofanya mazoezi naku keti kwa muda mrefu, sivizuri kwa afya ya moyo wako. Wataalam wa afya wame pendekeza kufanya mazoezi kwa muda wa nusu saa kila siku. Mbinu nzuri yaku anza niku tembea!

A man jogs in Brisbane
High-intensity interval training protects the heart and body against Type 2 diabetes, say experts. (AAP)

Kuvuta sigara

Una athari kubwa yakuwa na mshtuko wa moyo iwapo wewe ni mvuta sigara. Kuto vuta sigara ni moja ya mbinu nzuri yaku linda moyo wako. Unapo acha kuvuta sigara, athari ya ziada nayo hupungua.

A smoker enjoys a cigarette
Smoking costs $A1.4 trillion a year: study
AAP

Kujitenga na jamii na huzuni nyingi

Watu ambao hawana uhusiano na jamii, familia au marafiki wanaweza kuwa na athari kubwa ya matatizo ya moyo. Huzuni yakupindukia nayo inaweza changia katika hali hiyo. Shirika la Beyond Blue hupendekeza iwapo unakumbwa kwa huzuni yakupindukia kwa wiki mbili, zungumza na daktari wako, jamaa wako au mtu unaye mjua vizuri.

Hauwezi badili baadhi ya athari

Shirika la Heart Foundation lime chapisha baadhi ya athari ambazo hatuwezi dhibiti, athari hizo ni kama: miaka, historia ya familia au ukoo wako. Kwa mfano, watu kutoka ukanda wa India wana athari kubwa yaku kabiliwa kwa mshtuko wa moyo kuliko watu wengine.

Baadhi ya dalili ni gani?

Kuhisi usumbufu na uchungu kifuani

Dalili za hatari hutofautiana toka mtu mmoja kwa mwingine, dalili ya kwanza yakutafuta ni uchungu kifuani. Unaweza hisi kubanwa katika maeneo yakifua.

“Iwapo ni shambulizi la papo hapo, maumivu kifuani yatakuwa mengi bila mwisho. Utayahisi upande wa kushoto wa kifua, ila inaweza kuwa katika maeneo ya katikati. Maumivu hayo yata gonga pia katika eneo la taya na katika mkono wa kushoto" hiyo ni kwa mujibu wa mtaalam wa moyo Rob Perel kutoka shirika la Heart of Australia.

Maumivu mikononi, shingoni na mgongoni

Maumivu yanaweza sambaa katika sehemu tofauti za sehemu ya juu ya mwili. Unaweza hisi mikono yako inakuwa mizito au kuto tumika ipasavyo.

Kuhisi unakosa pumzi

Unaweza hisi unakosa pumzi. Dalili zingine zinaweza jumuisha hisia yaku banwa kooni, kichefuchefu, kutokwa jasho baridi na kuhisi kizunguzungu.

Utafanya nini?

An ambulance parks at St Vincent's Hospital
Man dies in Perth skydiving accident

Kitu cha kwanza chakufanya unapo kabiliwa kwa mshtuko wa moyo nikupigia simu nambari hii (000) na uombe gari la wagonjwa. “Wahudumu watakao jibu mwito wako, wata kupa dawa kwa jina la Aspirin watakapo wasili. Unastahili keti na upumzike, na uepuke kuweka shinikizo la ziada kwa moyo wako, hadi mtu mwingine atakapo kufanyia vipimo vya ziada naku kupa tiba." Hiyo ni kwa mujibu wa Rob Perel, mtaalam wa moyo kutoka shirika la Heart of Australia.

Pata maelezo ya ziada katika lugha yako.