Coming Up Tue 6:00 PM  AEDT
Coming Up Live in 
Live
Swahili radio

Taarifa mpya kuhusu COVID-19: ACT yaongeza muda wamakatazo kwa mara ya tatu

Mtu asukuma kifaa chenye bidhaa, katika eneo la maduka lililo tupu mjini Canberra, Jumatano, Agosti 25, 2021. Source: AAP Image/Lukas Coch

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa tarehe 14 Septemba 2021.

  • NSW yapanua malipo ya msaada wa COVID-19
  • Victoria yatangaza uwekezaji wa ziada kwa msaada wa afya ya akili
  • Makatazo jimbo la ACT  yaongezwa hadi 15 Oktoba
  • Queensland yarekodi kesi moja mpya ndani ya jamii

New South Wales 

NSW imerekodi kesi mpya 1,127 ndani ya jamii pamoja na vifo viwili.

Baada ya kutambuliwa kwa kisa cha COVID-19 jana katika eneo la halmashauri la Yass Valley, amri zakubaki nyumbani zita tumiwa kwa kila mtu anaye ishi au aliyekuwa katika eneo hilo tarehe 9 Septemba au baada ya tarehe hiyo.

NSW Health imewahamasisha wakaaji wa Young ambayo iko katika eneo la wilaya ya afya ya Murrumbidgee wajitokeze kufanyiwa vipimo, baada ya virusi hivyo kutambuliwa katika kiwanda cha taka. Kabla ya tukio hilo, palikuwa hapa jakuwa kesi yoyote katika jamii hiyo.

Msaad wa malipo ya Covid-19 yame panuliwa kwa wafanyakazi na jamii ambazo ziko katika hali mbaya, misaada hiyo inajumuisha uwekezaji kwa makundi yenye lugha na tamaduni mbali mbali.

Bonyeza hapa kufanya miadi yako ya chanjo.

Victoria

Victoria imerekodi kesi mpya 445 ndani ya jamii, pamoja na vifo viwili. Jimbo hilo kwa sasa lina shughulikia kesi 3,799, wakati 85% yao wana umri wa chini ya miaka 50.

Naibu kiongozi wa jimbo hilo James Merlino ametangaza mfuko wa uwekezaji wa dola milioni 22.1 kuunda huduma ya afya ya akili ndani ya jamii katika kanda ya Victoria na, maeneo ya jiji la Melbourne.

Pata hapa, kituo cha chanjo kilicho karibu yako.

Australian Capital Territory

Wilaya ya ACT imerekodi kesi mpya za maambukizi 22 ndani ya jamii. 

Makatazo katika wilaya hiyo yata ongezwa kwa muda wa wiki nne, mageuzi ya ziada kwa vizuizi yakitarajiwa kuanzia tarehe 17 Septemba, baadhi ya mageuzi hayo yakijumuisha biashara ndogo kuruhusiwa kuwadumia watu watano ndani ya biashara hiyo wakati wowote au, mtu mmoja kuwa na umbali wa mita nne na mteja mwenza ndani ya biashara husika.

Bonyeza hapa kutazama ustahiki wako kwa chanjo ya COVID-19 au kuona mipango yakuendelea mbele ya ACT.         

Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
  • Wakaaji wa Magharibi Australia wenye umri wa miaka 60 na zaidi, wata stahiki kupewa chanjo ya COVID-19 ya Pfizer kuanzia wiki ijayo.

 

 

 
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

NSW Safari & usafiri na Karantini
VIC Vibali vya safariWasafiri wa ng'ambo na Karantini
ACT Usafiri na Karantini
NT Safari na Karantini
QLD Safari na Karantini
SA Safari na Karantini
TAS Safari na Karantini
WA Safari na Karantini

Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:

COVID-19 Vaccination Glossary
Appointment Reminder Tool.


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 
Victoria 
Queensland 
South Australia 
ACT 
Western Australia 
Tasmania
Northern Territory 


Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 
Victoria 
Queensland 
South Australia 
ACT 
Western Australia 
Tasmania
Northern Territory

Source SBS/ALC Content
This story is also available in other languages.