Coming Up Sun 10:00 PM  AEDT
Coming Up Live in 
Live
Swahili radio

Taarifa mpya kuhusu COVID-19: Viongozi wamajimbo na wilaya walenga ramani yakupona COVID

Raia walio pata chanjo kamili, wachangia chakula nje mjini Sydney, Jumamosi, Septemba 25, 2021. Source: AAP Image/Dan Himbrechts

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 26 Septemba 2021.

  • Jimboni NSW, 59.25% ya umma unao stahiki ume pata chanjo kamili.
  • Jimboni Victoria, Geelong na Surf Coast kuondoka katika amri yakubaki ndani kuanzia usiku wa manane.
  • ACT yarekodi kesi mpya 25 ndani ya jamii.

New South Wales 

NSW imerekodi kesi mpya 961 ndani ya jamii pamoja na vifo tisa.

Dr Jeremy McAnulty kutoka idara ya afya ya NSW amesema idadi kubwa ya takwimu hizo zilikuwa katika vitongoji vya wasiwasi vinavyo jumuisha vitongoji vya; Guildford, Auburn, Punchbowl, Penrith, Bankstown, Liverpool na Bossley Park.

Kiongozi wa jimbo hilo Gladys Berejiklian amesema taarifa kuhusu jinsi jimbo hilo, lita safiri katika mchakato wakupona kutoka COVID unakamilishwa, na utatolewa wiki ijayo. Mamlaka wanapanga kutangaza baadae, hatua za afya kwa sehemu ya umma ambayo haija chanjwa.

Bonyeza hapa kuomba miadi ya chanjo yako leo. 

Victoria

Victoria imerekodi kesi mpya 779 ndani ya jamii pamoja na vifo viwili.

Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amesema baadhi ya vizuizi vita regezwa katika maeneo ya kanda ya Victoria na maeneo ya Jiji la Melbourne jimbo hilo litakapo fika kiwango cha 80%  ya watu ambao wame pokea dozi ya kwanza ya chanjo ya COVID, hatua ambayo inatarajiwa kufanyika Jumanne,  28 Septemba.

Umbali wakusafiri kutoka nyumbani kwa watu kuta ongezwa hadi 15 km na ruhusa ita tolewa kwa mazoezi ya nje, kucheza gofu, tennis pamoja na mpira wa vikapu, kwa vikomo vya idadi ya watu. Vizuizi vitaregezwa pia kwa wanao ongozwa na mwalimu kufanya mazoezi kwa watu ambao wamepata chanjo kamili.

Pata kituo cha chanjo kilicho karibu yako.                                                                           

Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita

  • Katika wilaya ya ACT, asilimia 85 ya umma wenye zaidi ya miaka 12 wamepokea dozi yao ya kwanza ya chanjo ya COVID-19.
  • Queensland haija rekodi kesi yoyote mpya ndani ya jamii.

 

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

NSW Safari & usafiri na Karantini
VIC Vibali vya safariWasafiri wa ng'ambo na Karantini
ACT Usafiri na Karantini
NT Safari na Karantini
QLD Safari na Karantini
SA Safari na Karantini
TAS Safari na Karantini
WA Safari na Karantini

Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:

COVID-19 Vaccination Glossary
Appointment Reminder Tool.


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 
Victoria 
Queensland 
South Australia 
ACT 
Western Australia 
Tasmania
Northern Territory 


Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 
Victoria 
Queensland 
South Australia 
ACT 
Western Australia 
Tasmania
Northern Territory

Source SBS/ALC Content
This story is also available in other languages.