Coming Up Sun 10:00 PM  AEDT
Coming Up Live in 
Live
Swahili radio

Wakati majira ya joto yanakaribia, Australia yapunguza vizuizi vya COVID-19 katika majimbo na vitongoji vyote

Baba akimsaidia binti yake kuvaa barakoa Source: Getty Images/Morsa Images

Vizuizi vya virusi vya corona kote Australia vinabadilika. Vinatofautiana kulingana na wapi unaishi kama jimbo na vitongoji hufanya mabadiliko kulingana na mahitaji na wasiwasi wao. Hapa tumeorodhesha hatua za sasa za majimbo na vitongoji.

Kwa taarifa zaidi za Kitaifa za SBS COVID-19BONYEZA HAPA

 • Taarifa hii inabadilika kila wakati lakini tunapendekeza pia uangalie vyanzo kwa kila mamlaka ya serikali za jimbo kwa taarifa kamili kiundani na matarajio.


Je! Majimbo na vitongoji vinalegeza vipi vikwazo vya COVID-19?


Victoria - Vigezo vyalegezwa

Vizuizi vya Victoria vinalegezwa kwa kasi tofauti huko Melbourne na vijini Victoria. 

 • Mjini Melbourne. Kuanzia saa 5:59 usiku siku ya Jumapili 27 Septemba vikwazo vya hatua ya pili vitaanza kwenye maeneo ya mjini Melbourne.

Ramani mpya: https://www.vic.gov.au/coronavirus-covid-19-restrictions-roadmap-metro-melbourne 

 • Mikoani Victoria. Kuanzia saa 5:59 usiku wa Jumatano tarehe 16 Septemba  vikwazo vya hatua ya tatu vitaanza kutumika katika maeneo ya mikoani Victoria. 

Ramani mpya: https://www.vic.gov.au/restrictions-roadmap-regional-victoria

Hatua kuelekea Kawaida ya COVID
(chini ya ushauri wa afya ya umma)

Hatua ya Kwanza - Imekwisha

Hatua ya pili - Mjini Melbourne (Septemba 28)

Bubbles za kijamii, kurudi kwa nguvu kazi na masomo.

• Amri ya kutotoka nje iliondolewa mjini Melbourne kuanzia saa 11 alfajiri Jumatatu tarehe 28 Septemba.
• Kutakuwa na faini kubwa kwa kukiuka sheria kuhusu wageni nyumbani kwako na mikusanyiko ya nje (angalia "Faini" hapa chini)
• Sababu nne za kuondoka nyumbani kwako zinabaki. Walakini vizuizi vingine vimebadilika:
- ununuzi wa chakula au vitu vingine muhimu
- mazoezi na shughuli za kijamii za nje na washiriki wa kaya yako au hadi watu watano (pamoja na wewe, na kutoka kwa kaya mbili) ikiwa tu hautasafiri zaidi ya 5km. Hii lazima iwe katika nafasi ya nje ya umma, na haitumiki kwa nyuma ya nyumba za watu au nafasi za nje zilizounganishwa na nyumba.
- kazi iliyoruhusiwa, na kwa madhumuni ya elimu. Hiyo ni pamoja na kupeleka watoto shule, chekechekea au huduma ya utunzaji wa masaa nje ya shule ambayo wameandikishwa.
- utunzaji, kwa sababu za huruma au kutafuta matibabu
• Kwa wanafunzi wa sekondari, kujifunza mtandaoni kunaendelea katika Hatua ya Pili wakati muhula wa 4 utakapoanza tena, isipokuwa kwa Mwaka 11-12.
• Katika Kipindi cha muhula wa 4, kuanzia 12 Oktoba, kutakuwa na kurudi kwa awamu za kusomoea madarasani kwa wanaojiandaa Daraja la 6, VCE (Y11-12 au wale wanaofanya masomo ya VCE au VCAL) na shule maalum.

Kwa kadiri uwezavyo, lazima ubaki nyumbani. Unapoondoka nyumbani, lazima utumie barakoa, isipokuwa uwe na sababu halali ya kutofanya hivyo.

Hatua ya Tatu 
Mikoani Victoria 16 Septemba)
Kuongezeka kwa ufunguzi wa michezo, burudani, sherehe na hafla maalum.

 • Hakuna vizuizi vya kuondoka nyumbani
 • Ukitumia muda na watu wengine, tumia muda nje ikiwezekana.
 • Mikusanyiko ya umma: hadi watu 10 kwa maeneo ya nje
 • Wageni wanaoruhusiwa majumbani ni kuanzia 1 kwa wakazi wa kaya (hadi watu 5)
 • Shule zinarudi kwa masomo ya darasani kwa muhula wa 4 kukiwa na hatua za kiusalama.
 • Huduma za usaidizi wa maeneo ya nje zimefunguliwa kwa watakaokaa tu
 • Maduka ya reja reja yamefunguliwa, isipokuwa kwa uangalizi binafsi (saluni za watengeneza nywele zimefunguliwa)

Mjini Melbourne (wakati muhimu kuanzalia vichocheo na ushauri wa afya ya umma)
Viwanda vikubwa vinarudi, kuongezeka kwa kufungua tena elimu, michezo, burudani, sherehe na hafla maalum.

Hatua ya Mwisho
Jimbo-zima (wakati muhimu kuanzalia vichocheo na ushauri wa afya ya umma)

Kuongezeka kwa idadi ya mikusanyiko na huduma.

COVID Kawaida
Hakuna vizuizi kwa mikusanyiko, wageni, huduma au mchezo.

"COVID Kawaida" inamaanisha:
- hakuna kesi mpya kwa siku 28
- hakuna kesi hai (jimbo-zima)
- hakuna milipuko yenye kutia wasiwasi nchi nzima

Waliotambuliwa na walio karibu nao

Watu wanaotambuliwa na virusi vya corona (na watu wanaoishi nao au walio karibu nao) wanatakiwa kujitenga wenyewe na kuingia karantini. Maelezo zaidi:  https://www.dhhs.vic.gov.au/sites/default/files/documents/202008/Diagnosed%20Persons%20and%20Close%20Contacts%20Directions%20%28No%2010%29%20-%2016%20August%202020.pdf  

Wageni mahospitalini

Kuna vikwazo vya hospitali katika umri, idadi ya wageni kwa mgonjwa, na kikomo kwa muda wa kutembelea wagonjwa: https://www.dhhs.vic.gov.au/sites/default/files/documents/202008/Hospital%20Visitor%20Directions%20%28No%2010%29%20-%2016%20August%202020.pdf

Faini

$ 5,000 faini inatumika kwa mikusanyiko isiyoruhusiwa

Kutokuvaa barakoa kunabeba adhabu ya $200

Wakazi wa Victoria watakaoshindwa kujitenga baada ya kupimwa na kukutwa na virusi au wakitambulika kuwa na ukaribu na wenye virusi watahitajika kulipa faini ya $4,957.

Kwa mujibu ya kesi, faini moja inaweza kuongezeka hadi $20,000.

Barakoa

Kufunikwa kwa uso kunabaki kuwa lazima, lakini sheria zimeimarishwa ili kuhakikisha kuwa barakoa lazima zivaliwe vizuri kufunika pua na mdomo.
Ngao za uso, ambazo hadi sasa zimeruhusiwa kama kifuniko cha uso, hazitaruhusiwa. Kutakuwa na kipindi cha neema kabla ya sheria kutekelezwa.

 Barakoa kwa watoto chini ya umri wa miaka 12 siyo lazima. Kwa maelezo zaidi kuhusu barakoa: https://www.dhhs.vic.gov.au/face-masks-covid-19

Msaada wa kifedha

Malipo ya maafa likizo ya janga ni mbadala wa malipo ya msaada wa wafanyakazi kwa virusi vya corona (COVID-19) toka serikali ya Victoria ambayo ni $1,500.

Taarifa zaidi: https://www.servicesaustralia.gov.au/individuals/services/centrelink/pandemic-leave-disaster-payment-victoria

 • Malipo ya jumla $300 kwa wafanyakazi wakazi wa Victoria, inajumuisha malipo ya wazazi na walezi, ambao watahitajika kujitenga wenyewe wakati wakisubiri upatikanaji wa majibu. 

Mwajiri

Kuanzia 28 Septemba 2020, vizuizi vingine vya kazi vitapunguzwa kote Victoria, chini ya "alama za kuchochea" kufikiwa na ushauri wa afya ya umma.

Mjini Melbourne ina viwango maalum vya vizuizi vya tasnia, inayohusiana na kesi ngapi za virusi vya corona (COVID-19) ziko katika jamii.

Shule 

Kurudi kwa shule kumepangwa kuanzia msimu wa 4 

• Wanafunzi wa shule maalumu na wanaojiandaa darasa la 6 watarudi kwenye masomo ya darasani kuanzia wiki ya Oktoba 12.
• Wale wanaofanya masomo ya VCE na VCAL watarudi kwa mitihani kuanzia Oktoba 5, na kisha kwa masomo kuanzia Oktoba 12.
• Kwa wanafunzi wa sekondari, masomo ya mtandaoni na rahisi yataendelea katika Hatua ya Pili wakati muhula wa 4 utaanza tena, isipokuwa kwa Mwaka 11-12.

Vituo vya chekechea

• Vituo vya utunzaji wa watoto vitakuwa wazi kwa watoto wote, na kikomo cha kilomita 5 hakitatumika.
• Mlezi mmoja ataruhusiwa kwa utunzaji wa watoto nyumbani.

Hali ya Dharura na Hali ya Maafa
Matangazo ya Hali ya Dharura ya Victoria na Hali ya Maafa yameongezwa kutoka Jumapili tarehe 13 Septemba hadi saa 11.59 jioni Jumapili tarehe 11 Oktoba 2020.

 Hali ya Maafa

 • Itawapa Polisi nguvu kubwa na kuruhusu mamlaka kusimamisha shughuli za Bunge.
 • Inaifanya serikali kuweka na kulazimisha katazo la kutoka ndani.
 • Kuteua Polisi kama maofisa wenye mamlaka, kuondoa mahitaji ya sasa ya Polisi kuwa na maafisa wa idara ya afya wakati wa kazi kama za ukaguzi wa vibali.

 

New South Wales

Sehemu za sasa zenye mlipuko wa maambukizi ya COVID-19 NSW:

https://www.nsw.gov.au/covid-19/latest-news-and-updates#latest-covid-19-case-locations-in-nsw

 • Mara moja jitenge hadi siku 14 baada ya wewe mara ya mwisho kuwepo kwenye eneo lolote lenye COVID-19.
 • Fanya vipimo hata ikiwa hauna dalili
 • Jisikilizie dalili za COVID-19 na urudie tena kupimwa ikiwa dalili zozote zitatokea
 • hata ikiwa hujakutwa na virusi, lazima ujitenge kwa siku 14.

Malipo kwa likizo za Maafa ya Janga

• Wafanyakazi wa New South Wales sasa wanastahiki malipo ya $1,500 kama malipo ya Likizo ya Maafa ya Janga ikiwa hawawezi kufanya kazi kwa sababu wanahitaji kujitenga au kurantini.
• Ni malipo ya mkupuo kuwasaidia wafanyakazi wakati wa siku zao za kujitenga za siku 14.

Maelezo zaidi: https://www.servicesaustralia.gov.au/individuals/services/centrelink/pandemic-leave-disaster-payment-new-south-wales

Kikomo cha mikusanyiko

Watu 20 nyumbani kwa nyumba na watu 20 kwenye mikusanyiko ya umma.

Huduma za kidini: kikomo cha watu kuhudhuria ukumbi wowote haitakiwi kuzidi watu 100, kulingana na sheria ya mita 4 za mraba.

Harusi: kikomo cha idadi ya watu hakitakiwi kuzidi watu 150 kulingana na sheria ya mita 4 za mraba na usajili wa biashara salama kwa COVID.

Mazishi na shughuli za ukumbusho: kikomo cha idadi ya watu kinatakiwa kuwa kwa mtu mmoja kwa mita 4 za mraba au watu 100.

Biashara na shughuli za burudani:

NSW gym na sehemu zingine za mazoezi lazima:

 • kujiandikisha na kuwa na mpango salama wa COVID
 • kuwa na mpango salama wa usafi wa COVID-19 wakati wote (mfanyakazi mmoja wa usafi wa COVID-19 ambaye atakuwa amevaa nguo za kujikinga na atakuwa mwajibikaji wa nyanja zote za mpango salama wa COVID-19.

Mabaa, mahoteli, migahawa, sehemu za chakula na vinywaji, wazalishaji pombe, wauzaji, wauzaji wa pombe, vilabu vilivyosajiliwa, baa ndogo na makasino:

 • kikomo cha maombi ya kukusanyika kuwa kwa watu 10 tu.
 • Rekodi ya kigitali lazima kutengenezwa katika kpindi cha masaa 24. 
 • harusi na sherehe za makampuni zina kikomo cha watu 150, ikizingatiwa sheria ya mita nne za mraba.
 • mazishi na sehemu za dini kikomo cha watu 100.

Kusafiri

NSW imeweka dharura ya muda mfupi kufunga mipaka kati yake na jimbo la Victoria.

Watu wanaorejea New South Wales kutoka Victoria wanalazimishwa kujitenga kwa wiki mbili katika mahoteli kwa gharama zao wenyewe. 

Wakazi wa maeneo ya mpakani wanaweza kuomba kibali NSW kupitia (https://disasterassistance.service.nsw.gov.au/bcpermit/borderCheck) kuvuka mpaka kuingia NSW, kukiwa na masharti kadhaa kwa wakazi wa Victoria wa mpakani.

 • Ameruhusiwa kuingia na kubaki NSW kwa kazi tu, elimu, matibabu au huduma ya afya, au kutoa au kupokea huduma kwa mtu aliye katika mazingira hatarishi, na
 • Lazima asisafiri kwenda sehemu yoyote ya NSW ambayo iko nje ya eneo la mpaka na
 • Lazima asiingie NSW ikiwa amesafiri huko Victoria nje ya eneo la mpaka kati ya siku 14 zilizopita.

Angalia hapa kama unaishi kwenye eneo la mpaka: https://www.service.nsw.gov.au/border-zone-address-check

Gharama za hoteli za karantini, ambazo ziliondolewa kwa mwezi mmoja , zimerudishwa kutumika kuanzia 11 Septemba.

Watu watakaosafiri kwa ndege kuingia New South Wales kutoka nje ya nchi pia wanalazimika kuingia wiki mbili za hotel karantini kwa gharama zao wenyewe. (AUD 3,000)  https://www.nsw.gov.au/media-releases/nsw-to-charge-returned-international-travellers-for-hotel-quarantine

Vifungu maalumu vimetengwa kwa:

 • wakazi wa mipakani
 • watu wanaojishughulisha na kutoa huduma muhimu
 • wakazi wa majimbo mengine wanaopitia NSW.

Kwa maelezo zaidi: https://www.nsw.gov.au/covid-19/what-you-can-and-cant-do-under-rules/border-restrictions

 • Wasafiri kutoka majimbo mengine wanaruhusiwa kutembelea NSW kwa mapumziko lakini watatakiwa kufuata sheria za majimbo yao wakati wakirudi huko.
 • Watu ambao wanashindwa kufuata sheria wanaweza kukabiliwa na kifungo cha miezi sita au faini ya hadi dola 11,000 au zote mbili.
 • Sehemu nyingi za kuegesha magari ya mapumziko(caravan parks) na maeneo ya kupiga kambi yamefunguliwa. Wasafiri wanaopanga kutembelea hifadhi za taifa wanapaswa kuangalia tovuti ya www.nationalparks.nsw.gov.au 
 • Kutembelea vituo vya kulelea wazee au huduma ya afya imekatazwa.

Kwa maelezo zaidi: 

Shule

 • Mwanafunzi yoyote mwenye dalili za COVID-19 haruhusiwi kurudi shuleni hadi hapo atakapopima na kukutwa hana ugonjwa huo.
 • Tafrija za shule, kucheza mziki, mahafali na shughuli zingine za kijamii haziruhusiwi.
 • Mashule zitafanya mkutano wa wanafunzi wa mwaka 12 bila ya wazazi kugundua kumaliza shule kwa wanafunzi hao.
 • Watoa huduma tu ambao ni muhimu katika utoaji wa mitaala wanaweza kuendelea kutoa huduma na programu.
 • Shughuli baina ya shule na shule lazima zibaki ndani ya jamii au eneo la karibu.
 • Wazazi/walezi na wageni wengine wasio muhimu hawaruhusiwi kwenye eneo la shule.
 • Kuimba kwa vikundi vyote (kwaya) na/au shughuli zingine za kuimba, pamoja na utumiaji wa vyombo vya upepo katika mipangilio ya kikundi, hairuhusiwi.
 • Kantini na maduka ya sare za shule yanaweza kufunguliwa kwa hiari ya mwalimu Mkuu.
 • Safari za siku kwenda kwenye maeneo ya nje bila ya kuwa na mahitaji ya kujitenga na watu zinaweza kufanyika.

Kwa maelezo zaidi kwa familia tembelea: https://education.nsw.gov.au/covid-19/advice-for-families

Taarifa zaidi za NSW: https://www.nsw.gov.au/covid-19

Queensland

Shughuli za kishule

Shughuli za shule rasmi zimefutwa, kama vile hafla zilizopangwa na matamasha kwenye tamasha la kila mwaka la Gold Coast.
Vikundi vidogo vya vijana wanaruhusiwa kufanya maombi ya makao katika maeneo karibu na mahali walipokuwa wakiishi, lakini hafla rasmi ya Schoolies imefutwa.

Kikomo cha mikusanyiko

Mikusanyiko katika nyumba na nafasi za umma umepunguzwa hadi watu 30, isipokuwa kwa Sehemu zilizokatazwa: https://www.qld.gov.au/health/conditions/health-alerts/coronavirus-covid-19/current-status/restricted-areas-covid-19/queensland-covid-19-restricted-areas-31-August-2020

 • Jiji la Brisbane
 • Jiji la pswich
 • Mji wa Logan 
 • Mkoa wa Scenic Rim
 • Mkoa wa Somerset 
 • Mkoa wa Lockyer Valley
 • Mkoa wa Moreton Bay 
 • Mji wa Redland 
 • Cherbourg Aboriginal Shire
 • Mji wa Gold Coast 
 • Mkoa wa Goondiwindi 
 • Mkoa wa South Burnett
 • Southern Downs
 • Mkoa wa Toowoomba
 • Mkoa wa Western Downs.

Vizuizi vitawekwa kwa:

Vituo vya usaidizi kwwa wazee: Vikwazo vya kutembelea: https://www.health.qld.gov.au/system-governance/legislation/cho-public-health-directions-under-expanded-public-health-act-powers/aged-care

Watembeleaji Hospitali: https://www.health.qld.gov.au/system-governance/legislation/cho-public-health-directions-under-expanded-public-health-act-powers/hospital-visitors-direction

Matembezi na Mikusanyiko. Kikomo cha juu watu 10 katika maeneo yaliyokatazwa na watu 30 katika sehemu zisizo na makatazo: https://www.health.qld.gov.au/system-governance/legislation/cho-public-health-directions-under-expanded-public-health-act-powers/movement-gathering-direction

Huduma za makazi kwa walemavu: https://www.health.qld.gov.au/system-governance/legislation/cho-public-health-directions-under-expanded-public-health-act-powers/disability-accommodation-services

Kwa maelezo zaidi kuhusu maeneo:  https://www.qld.gov.au/health/conditions/health-alerts/coronavirus-covid-19/current-status/restricted-areas-covid-19

Biashara na burudani

Hadi Desemba 2020 wafanyakazi wa kawaida ambao hawatapa malipo ya likizo za kuumwa wanapewa $1,500 kutoka serikali ya Queensland ikiwa watapima na kukutwa na virusi vya corona. Pia inashughulikia wafanyakazi ambao hawastahili mpango wa JobKeeper, ambao uko zaidi kwa wafanyakazi wa kawaida wa muda mrefu.

Sheria ya mtu mmoja kwa mita za mraba 4 inatumika kwa:

Idadi ya wateja katika biashara (kwa kumbi ndogo chini ya mita za mraba 200, mtu mmoja kwa kila mita 2 za mraba hadi watu 50)

Makumbusho, nyumba za sanaa, maktaba na sehemu za kihistoria.

Michezo, burudani na mashirika ya mazoezi ya mwili wakiwa wanafuata Mpango wa COVID Salama.

Ushindani na makutano ya kawaida ya kimwili kwenye viwanja vya michezo

Vituo vya michezo vya ndani

Hadi watazamaji 25,000 au 50% ya uwezo (yoyote ambayo ni ndogo) katika Kituo Kikuu cha Michezo cha Queensland, pamoja na Mpango Salama wa COVID

Sehemu za matamasha, maonyesho na majumba ya kumbukumbu (au hadi uwezo wa 50%) na Mpango Salama wa COVID.

Vijijini

Watu 50 wanaruhusiwa wakati wowote kwa kula chakula ndani (Huku zikifuata utaraibu wa mpango wa COVID salama).

 • Mahoteli, migahawa, mabaa, vilabu vilivyosajiliwa na vyenye leseni, vilabu vya RSL na mahotel kwa wakazi wa maeneo hayo tu (lazima waonyeshe uthibitisho wa ukazi) - hakuna ruhusa kwa sehemu za kamali.
 • Kusafiri kwa matembezi ni vjijini tu ikiwa unaishi huko vijijini.

Jamii za asilia - maeneo ya vizuizi vya mlipuko

Serikali za Jimbo na Viongozi wa Asili wamekubaliana juu ya mpango wa hatua tatu wa kupunguza vikwazo katika maeneo yaliyotengwa ya Serikali ya Shirikisho.

Jamii zilizotengwa zimebadilisha kutoka kwa vikwazo vya sasa vya dharura kishirikisho hadi mpangilio wa majimbo.

Vizuizi vya kuwekewa mipaka ya kuingia katika jamii za asili za Kiaborigino vimeondolewa, na maeneo ya Burke na Cook Shires yawe chini ya vifungu sawa na maeneo mengine ya Queensland chini ya ramani ya mwenendo wa kulegeza vizuizi: https://www.datsip.qld.gov.au/resources/datsima/covid/remote-communities-roadmap.pdf

Vikwazo vya kusafiri

 • Kuanzia saa 7 usiku Alhamis, Octoba 1 mipaka ya maeneo ya QLD itaongezwa kujumuisha Byron, Ballina, Lismore, Richmond Valley and maeneo ya Glen Innes.
 • Wakazi wa mipakani wanaweza kuomba kibali cha mipaka na kusafiri ndani ya QLD kwa shughuli yoyote, na wakazi wa Queensland wanaweza safiri katika maeneo hayo. 
 • Mipaka ya Queensland kwa sasa imefunguliwa kwa wakazi wa Canberra, bila kupitiakujitenga kwa siku 14 kwa hoteli karantini.
 • Mtu yoyote aliyekuwa kwenye maeneo yaliyotangazwa rasmi kuwa yenye mlipuko mkubwa wa COVID-19 katika kipindi cha siku 14 zilizopita, ukijumuisha na Victoria, hawaruhusiwi kuingia Queensland.
 • Wakazi wa Queensland wanaorejea, watapelekwa kwenye karantini kwa siku 14 kwa gharama zao wenyewe.
 • Mtu yeyote anayesafiri kutoka Australia Magharibi, Australia Kusini, Tasmania na Jimbo la Kaskazini anaweza kuingia Queensland akilazimika kumaliza na kutia saini tamko la mpaka na kujitolea kuwepo kwa upimaji wa COVID-19 ikiwa ataonyesha dalili.Hivi ni jinsi ya kuomba kibali: https://www.covid19.qld.gov.au/government-actions/border-closing

Shule

 • Wanafunzi wote wanahudhuria shule.

Taarifa zaidi za Queensland: https://www.qld.gov.au/covid-19/government-actions/roadmap-to-easing-queenslands-restrictions

Australia Kusini

Kikomo cha mikusanyiko 

 • Mikusanyiko kwa nyumba binafsi haitatakiwa kuzidi watu 50.
 • Mikusanyiko katika maeneo binafsi, zaidi ya nyumba binafsi (ndani au nje) kwa sasa kuna vikwazo kwa kutokuwa na watu zaidi ya 100.
 • Baa na mahoteli: wanaweza kuhudumia pombe kwa wateja waliokaa, mbali na eneo la baa au sehemu ya kuagizia.
 • Eneo la kusafiri kwa kilomita 40 kuvuka mipaka kijamii ndani ya Victoria na Australia Kusini limerejeshwa
 • Watu wanaosafiri kwenda SA kupitia viwanja vya ndege vya Sydney au Canberra kutoka Australia Magharibi, Wilaya ya Kaskazini, Queensland au Tasmania hawastahili tena kujitenga wenyewe kwa siku 14.

Biashara na burudani 

Biashara, shughuli na mikusanyiko inaruhusiwa: https://www.covid-19.sa.gov.au/emergency-declarations/public-activities

Biashara na shughuli za umma zilizo na Mpango uliopo wa COVID-Salama hazihitaji kukamilisha mpango mpya, isipokuwa  unafungua nafasi au maeneo zaidi.

Biashara na shughuli za umma zilizoelezewa ambazo hazina Mpango salama wa COVID lazima zikamilishe mpango kabla ya kuanza kufanya kazi: https://www.covid-19.sa.gov.au/recovery/create-a-covid-safe-plan

Vikwazo vya kusafiri

 • Usafiri wa kikanda unaruhusiwa ndani ya Australia Kusini
 • Mtu yoyote haingii Australia Kusini, ikiwa unatokea Victoria, hata Waustralia Kusini.
 • Wasafiri muhimu tu wanaweza kuingia Australia Kusini kutoka Victoria, wakijumuishwa wanachama wa jumuiya za mipakani.
 • Wanajumuiya wa mpakani katika mpaka wa Australia Kusini/Victoria lazima waombe tena kibali cha aina tofauti cha Msafiri Muhimu. Ikiwa wana hali ya kusafiri iliyoidhinishwa, hawana haja ya kuomba idhini mpya ikiwa ni:

- wanafanya mtihani wa mwaka wa 11 au 12 elimu ya juu katika shule za sekondari.

- wakimsafirisha mtu kwa kutumia usafiri binafsi ambaye anasoma elimu ya juu ya mwaka wa 11 au 12.

- mfanyakazi wa kilimo/viwanda mwenye nyumba karibu na mpaka wa SA/VIC.

 • Wasafiri kutoka Jimbo la Kaskazini, Queensland, Tasmaniana Australia Magahribi wanaruhusiwa kuingia Australia Kusini moja kwa moja bila vikwazo.
 • Wasafiri kutoka NSW wanaruhusiwa kuingia SA kuanzia usiku wa Jumatano 23 Septemba, na hawatahitaji kujitenga wenyewe kwa siku 14.
 • Katika kipindi cha siku 14 lazima ukae nyumbani (au chumba cha hotel) na usitoke isipokuwa unahitaji huduma ya matibabu ya haraka.
 • Mpaka wa Australia Kusini umefunguliwa kwa wakazi wa Canberra, na wasafiri hawahitaji kujitenga kwa siku 14 wakiwasili.
 • Wasafiri wa nje ya nchi watahitajika kujitenga wenyewe. Pia, ikiwa umekutwa na virusi au ulikuwa karibu na mtu mwenye virusi.
 • Ikiwa unapanga kusafiri kuingia Australia Kusini, jaza fomu ya usajili wa kusafiri kuvuka mpaka siku 3 kabla hujaondoka, haijalishi unatokea wapi:https://www.police.sa.gov.au/online-services/cross-border-travel-application

Shule

Shule za Australia Kusini zimefunguliwa tangu mwanzoni mwa muhula wa 2 na wanafunzi wanahimizwa kuhudhuria, kufuatia miongozo ya muhula wa 2 ya uendeshaji kwa shule za umma za Australia Kusini.

Taarifa zaidi: https://www.covid-19.sa.gov.au/recovery

 

Australia Magharibi

Malipo ya maafa ya COVID-19 

Tangu tarehe 16 Septemba 2020, Australia Magharibi waliweka malipo ya likizo ya janga $1,500 kupatikana kwa wafanyakazi walioathiriwa na COVID-19 ambao hawatoweza kufanya kazi.

Waustralia Magharibi wanaostahiki watapokea malipo ya jumla $1,500 kila baada ya siku 14 ambazo hawafanyi kazi.

Malipo yanaweza kupokewa mara mbili ikiwa maafisa wa wizara ya afya watawaamuru kujitenga kwa zaidi ya siku 14, au zaidi ya wakati mmoja. Taarifa zaidi: https://www.servicesaustralia.gov.au/individuals/services/centrelink/pandemic-leave-disaster-payment-western-australia

HATUA YA 4

 • Vikwazo vya COVID-19 Australia Magharibi sasa viko kwenye hatua ya 4 (kayi ya hatua 6) ya ramani za jimbo.
 • Hatua ya 5 imesogezwa mbele hadi tarehe 24 Agosti, lakini washauri wa afya huenda wakashauri kusogeza mbele zaidi.
 • Ramani ya Australia Magharibi kwa lugha ya Kiingereza na lugha zingine:https://www.wa.gov.au/government/publications/covid-19-roadmap
 • Vikwazo vyote vya mikusanyiko na sheria za 100/300 zimeondolewa.
 • kikomo cha mikusanyiko kinaamuliwa na Waustralia Magharibi kimepunguzwa kwa sheria ya mita za mraba 2 (kwa wafanyakazi wa kumbi zinazoingiza watu zaidi ya 500).
 • kuondolewa kwa mahitaji ya huduma ya kukaa katika biashara za chakula na sehemu zilizo na leseni.
 • hakuna mahitaji ya kusajili wateja katika mahotel, migahawa na baa. 
 • matamasha yote yameruhusiwa kasoro yenye idadi kubwa, yenye majukwaa mawili ya muziki kwenye tamasha.
 • maonyesho kwa wasiokaa yameruhusiwa katika matamasha kama vile kumbi za muziki, sehemu za muziki mubashara, baa na vilabu vya usiku.
 • sehemu ya michezo ya casino inafunguliwa tena chini ya makubaliano ya muda mfupi.

 

Vikwazo vya kusafiri

Hauruhusu kuingia Australia Magharibi (WA) isipokuwa wewe ni msafiri uliyeruhusiwa: https://www.wa.gov.au/government/document-collections/covid-19-coronavirus-state-of-emergency-declarations#travel-and-border-state-wide

Wasafiri ambao walikuwa Victoria au New South Wales katika siku 14 zilizopita wanaruhusiwa kuingia WA, isipokuwa wakiangukia katika vipengele vya ruhusa: https://www.wa.gov.au/government/publications/victoria-and-new-south-wales-arrivals-frequently-asked-questions

Kusafiri kunaruhusiwa katika eneo lote ndani ya Australia Magharibi, ukijumuisha kuingia mkoa wa Kimberley. Fursa ya kufika eneo la vijijini la jumuiya za Waaborigino bado ni marufuku.

Shule

 • Shule za umma za Magharibi mwa Australia zilifunguliwa mwanzoni mwa muhula wa 2 kwa familia zote ambazo huchagua kupeleka watoto wao shuleni.
 • Kwa wanafunzi ambao wanajifunzia nyumbani, vifurushi vya elimu ya mbali na rasilimali zinatolewa.
 • Wazazi/walezi wanaweza kuingia eneo la shule kushusha au kupakia watoto.

Kwa maelezo zaidi kuhusu shule za Australia Magharibi tembelea: https://www.wa.gov.au/organisation/department-of-the-premier-and-cabinet/covid-19-coronavirus-education-and-family-advice 

Taarifa zaidi ya WA: http://www.wa.gov.au/covid19roadmap

 

Tasmania

Malipo ya likizo kwa Maafa ya Janga

Wafanyakazi wa Tasmania sasa wanastahili malipo ya likizo kwa Janga ya $1,500 ikiwa hawawezi kufanya kazi kwa sababu wanahitaji kujitenga au kukaa karantini.

Ni malipo ya mkupuo ya kusaidia wafanyakazi wakati wa kipindi chao cha kujitenga cha siku 14.

Taarifa zaidi: https://www.servicesaustralia.gov.au/individuals/services/centrelink/pandemic-leave-disaster-payment-tasmania

Kikomo cha mikusanyiko

 • Majumbani: hadi watu 20 kwa wakati wowote, haijumuishi wakazi wa humo.
 • Idadi ya kikomo cha watu ukijumuisha na wafanyakazi, wanaojitolea, watoto na vichanga.

Biashara na burudani

 • Idadi ya watu wanaotambuliwa kwa uwiano wa eneo: kikomo cha watu 250 ndani ya nyumba na watu 1000 nje (kuanzia Ijumaa 25 Septemba)
 • Kikomo cha juu cha uwiano ni mtu mmoja kwa mita 2 za mraba: https://www.coronavirus.tas.gov.au/families-community/gatherings-density-and-physical-distancing
 • Pale ambapo idadi ya watu wanaoruhusiwa kulingana na kikomo cha uwiano ni chini ya kikomo cha kukusanyika, idadi ya chini inatumika.
 • Watu wanaohudhuria hafla katika eneo lenye leseni wanaweza kuzunguka kwa uhuru, lakini lazima waketi wakati wakinywa pombe.
 • Gym zimefunguliwa, kukiwa na mipango salama ya COVID ikijikita kwa eneo, umbali toka mtu hadi mtu, ufuatiliaji kwa walioambukizwa, kusafisha na usafi 

Taarifa zaidi kuhusu vikwazo vya biashara: https://www.coronavirus.tas.gov.au/business-and-employees/business-restrictions

Vikwazo vya kusafiri

 • Hali ya hatari katika jimbo imeongezwa hadi tarehe 26 October 2020.
 • 1 Desemba 2020 ndio tarehe iliyopangwa kuelegeza mipaka ya Tasmania
 • Unaweza kusafiri na kukaa popote ndani ya Tasmania, lakini lazima utimize masharti ya vikwazo juu ya mikusanyiko na kutembea majumbani.
 • Kurejea kutokea Queensland: Watasmania wanaoerejea ambao wametumia muda maeneo ya Brisbane mjini, mjini Ipswich na jiji la Logan wanahitajika kukamilisha karantini kwa siku 14 katika makazi yaliyotengwa na serikali.

Pata taarifa za kusafiri Tasmania: https://www.coronavirus.tas.gov.au/travellers-and-visitors/coming-to-tasmania

Mchakato wa hatua tatu kupunguza vizuizi vya mpaka:

Hatua ya 1
- Kuanzia Jumapili 20 Septemba: wafanyakazi wa FIFO wa Tasmania ambao walikuwa hawako kwa muda mrefu wakifanya kazi katika maeneo yenye hatari kidogo kuruhusiwa kwenda nyumbani bila karantini -ikiwa watarudi moja kwa moja kutoka majimbo yao salama bila kutumia wakati huko Victoria au maeneo mengine yenya hatari zaidi..
- Ruhusu kwa wafanyakazi wa muda mfupi kuingia Tasmania, chini ya hali salama ya COVID, kwa msimu ujao.

Hatua ya 2
Mwisho wa Oktoba 2020 - Mdhibiti wa Jimbo atazingatia kutangaza tarehe ya kupunguza vizuizi vya mpaka kwa kutumia mamlaka za COVID-Salama na vizuizi vichache kwa majimbo ya SA, WA, NT, Queensland, ACT, na labda NSW.

Hatua ya 3
Idara ya Afya ya Umma itatoa ushauri ikiwa Tasmania iko tayari kwa tarehe 1 Desemba kumaliza vizuizi vya mpaka na Victoria au maeneo mengine yenye hatari.

Usajili wa Safari Mtandaoni

 • Yeyote anayetaka kusafiri kwenda Tasmania kutoka sehemu nyingine ya nchi au nje ya nchi lazima ajiandikishe kwenye mfumo wa usajili wa kusafiri mtandaoni unaitwa G2G PASS kupitia https://www.g2gpass.com.au, kabla ya kuwasilisha ombi la ruhusa ya kuingia.

 • Unatakiwa kujaza vizuri progamu ya Good to Go katika kipengele cha ulikuwa wapi katika siku 14 zilizopita na faini inayoweza fikia hadi $16,800 au hadi miezi 6 jela kwa wale watakaotoa taarifa za uongo.

Kwa maelezo zaidi: https://www.coronavirus.tas.gov.au/ 


Shule

 • Wanafunzi wote wanahudhuria mashuleni.

Taarifa zaidi: https://www.coronavirus.tas.gov.au/

 

Jimbo la Kaskazini 

Kikomo cha mikusanyiko

Hakuna vikwazo vyovyote vya mikusanyiko NT, lakini watu wameombwa kufuata sheria za kukaa umbali wa mita 1.5 katika maharusi na mazishi kunaruhusiwa

Biashara na starehe

Biashara zote zinaruhusiwa kufunguliwa, hata michezo.

 • Michuano ya jumuiya au mashindano ya michezo yenye mashabiki waliokaa tu kimpangilio ulioruhusiwa. Ikiwa ni zaidi ya watu 500, tamasha au mchezo huo utahitajika kufuata mpango mwingine salama wa COVID-19. 
 • Matukio makubwa yatakuwa yakihidhinishwa kimsingi wa kesi kwa kesi.

 

Vikwazo vya kusafiri

 • Kuwasili eneo la Kaskazini kutoka nchi za nje, wanaelekezwa kwa dhamana ya lazima inayosimamiwa karantini hapo Howard Springs na watalipishwa $2,500

Wanaowasili kutoka mikoani Jimbo la Kaskazini

Ikiwa siyo kutoka maeneo yaliyotangazwa kuwa hatari, hautahitajika kujitenga mwenyewe. Orodha ya maeneo hatari: https://coronavirus.nt.gov.au/travel/quarantine/hotspots-covid-19

Kuanzia Ijumaa 9 Octoba, Jimbo la Kaskazini litaiondoa Sydney kutoka katika orodha ya maeneo hatarishi, ikiwa NSW itaendelea kupungza kesi za maambukizi.

Kutoka au kupitia maeneo hatari yaliyotangazwa katika siku 14 zilizopita lazima wapitie siku 14 za karantini inayosimamiwa kwa lazima: https://coronavirus.nt.gov.au/travel/quarantine

Wanaowasili wote kutoka mikoani katika jimbo jilo, lazima wajaze fomu ya ruhusa ya kuvuka mpaka hadi masaa 72 kabla ya kuwasili

 • Endelea kufuatilia mara kwa mara sehemu zilizotangazwa kuwa hatarishi

Kwa maelezo zaidi kuhusu hatua 6: https://coronavirus.nt.gov.au/travel/quarantine

Shule

 • Wanafunzi wote wa Jimbo la Kaskazini wamesharudi mashuleni
 • Ambapo familia zitakazochagua kutompeleka mtoto wao shule, mtoto lazima awe anajifunzia kutoka nyumbani.

Maelezo zaidi ya shule za Jimbo la Kaskazini: https://education.nt.gov.au/publications/information-for-term-2-2020?SQ_VARIATION_814972=0

Ramani za mwenendo wa Jimbo la Kaskazini: https://coronavirus.nt.gov.au/steps-to-restart/roadmap-new-normal

 

Jimbo la Mji Kuu wa Australia

Kikomo cha mikusanyiko

Kwa maelezo zaidi juu ya mikusanyiko:  https://www.covid19.act.gov.au/protecting-yourself-and-others/groups-and-gatherings

Biashara na burudani

 • Mashindano ya michezo yenye kuruhusu kugusana, ikijumuisha kucheza muziki na sanaa za mapigano, imeanza (wakirudi kucheza huku wakifuata mpango wa mazingira salama wa COVID). https://www.covid19.act.gov.au/what-you-can-do/faqs-changes-to-restrictions/sport-recreation-pools
 • Mashindano na uogeleaji unaweza kuanza kwa kujipanga mstari katika mikusanyiko kwa kikomo katika mabwawa ya kuogelea na hakuna kikomo cha idadi ya waogeleaji kwenye mstari mmoja.
 • Miongozo ya biashara ya ACT: https://www.covid19.act.gov.au/business-and-work
 • Kuanzia 18 Septemba 2020, hotel, migahawa na baa za Camberra zinaweza kuingiza watu 25 haijalishi ukubwa wa ukumbi.
 • Baa, na vilabu vinaweza kutoa pombe kwa wateja walioketi katika vikundi vya hadi watu 10 kwa maombi ya meza au meza bila kutoa chakula.
 • Mafunzo kamili ya michezo ya kukutana, kucheza muziki na sanaa ya kupigana kwa sasa zinaruhusiwa.
 • Zifuatazo zinaweza kufunguliwa, ukizingatia sheria ya mtu mmoja kwa mita 4 za mraba kwa watu 100 (pamoja na wafanyakazi):

- Sehemu za ibada na sherehe za kidini.
- Sinema na sehemu za maonyesho
- Vituo vya burudani vya ndani na nje, uwanja wa michezo, na vituo vya   kucheza
- Gyms, vilabu vya afya, mazoezi ya mwili, densi
- Mabwawa ya kuogelea
- Michezo ya Jumuiya na shughuli za kupangwa za michezo
- Kwaya, bendi na orchestra
- Huduma za kibinafsi,(urembo na saluni za kucha, tatoo, sehemu na kukandwa kandwa, n.k)
- vituo vya kuegesha magari ya mapumziko, viwanja vya kambi na tovuti za kambi

Ulinzi wa Huduma za Afya

Chombo kipya cha uchunguzi cha kidijitali kinapatikana ili kujua ikiwa ni salama kwa mtu kuingia kituo cha afya. Kinajumuisha kujibu mfululizo wa maswali rahisi. Alama ya vyema ya kijani au nyekundu litaonyesha ikiwa ni salama au siyo salama kuingia: https://screening.covid19.act.gov.au/

Vizuizi vikali vya wageni katika vituo vya afya:
Mgeni mmoja kwa kila mgonjwa, kwa siku.
Mtoto mchanga au watoto waliolazwa wanaweza kuwa na mzazi/mlezi mmoja.

Shule

Kusafiri:

 • Wakazi wa ACT wanaokwenda katika majombo mengine na vitongoji: Serikali ya ACT inasisitiza watu kutokusafiri katika maeneo ambapo mlipuko wa COVID-19 unaendelea. Kwa sasa inajumuisha kote Victoria na sehemu kubwa ya Sydney.
 • Kusafiri kwenda ACT kutoka NSW au Queensland: Watu ambao wamekuwa katika eneo kubwa la Sydney wanashauriwa kutotembelea au kufanya kazi katika mazingira hatarishi, pamoja na vituo vya utunzaji wa wazee, hospitali na magereza, kwa muda wa siku 14 baada ya kuondoka Eneo kubwa la Sydney.
 • Hakuna sharti kwa watu hawa kujitenga.
 • Kusafiri kwenda ACT kutoka Victoria: Mtu yeyote (isipokuwa wakaazi wa ACT) anayesafiri kutoka Victoria atakataliwa kuingia ACT isipokuwa akipewa msamaha na idara ya Afya ACT.
 • Kuingia ACT kutokea Victoria sasa kunawezekana tu kupitia Uwanja wa Ndege wa Canberra, kwa ndege.
 • Wakazi wa ACT kutoka Victoria wanahitajika kuingia karantini hadi siku 14 baada ya kuondoka Victoria, na kuwajulisha maafisa masaa 72 kabla ya tarehe ya kusafiri iliyokusudiwa.

 

 • Watu nchini Australia lazima wakae umbali wa mita 1.5 kutoka kwa mwingine. Angalia vizuizi vya makutano katika jimbo lako.
 • Wakazi wa Melborne mjini wako katika hatua ya 4 ya vikwazo na lazima wafuate katazo la kutotoka nje kati ya saa 2 usiku na saa 11 alfajiri. Orodha kamili ya vikwazo inaweza patikana hapa: https://www.dhhs.vic.gov.au/updated-restrictions-announcement-2-august-covid-19
 • Ikiwa unajihisi na dalili za homa au mafua, panga hatua za upimaji kwa kumpigia daktari wako au kuwasiliana na namba ya watoa huduma za maelezo ya afya kitengo cha virusi vya corona kupitia 1800 020 080.
 • SBS imejitolea kuziarifu jamii tofauti za Australia juu ya maendeleo ya hivi karibuni ya janga la COVID-19. Habari na maelezo yanapatikana kwa lugha 63 kupitia sbs.com.au/coronavirus 
Source SBS