Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Binti wa Kiindonseia akamatwa juu ya tuhuma za kumuua rafiki yake kwa sumu

Binti wa Kiindonesia amekamatwa akituhumiwa kumuua rafiki yake kwa sumu ambaye walisoma naye hapa Australia.

Wayan Mirna Salihin

Source: Facebook

Wayan Mirna Salihin mwenye umri wa miaka 27, alifariki dunia mjini Jakarta mapema mwzi huu baada ya kunywa kahawa na rafiki zake wanaojulikana kwa majina ya Jessica Kumala and Hani.

Inaaminika kuwa, kinywaji chake kiliwekewa sumu aina ya cyanide.

Kufuatia wiki kadhaa za upelelezi, polisi wa Jakarta, leo hii wamemkamata Bi Jessica Kumala.

Mabinti hao watatu walisoma pamoja masuala ya ubunifu, katika chuo cha Billy Blue mjni Sydney na pia chuo kikuu cha Teknolojia Swinburne huko Melbourne.

Imeelekwa kuwa Polisi wa shirikisho Australia wameliambia jeshi la Polisi Jakarta watatoa msaada wa ushirikiano kusaidia kesi hiyo.


1 min read

Published

Updated

By Zara Zaher, Frank Mtao

Source: SBS News



Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now