Tuku alikuwa mmoja wa walio pinga uongozi wa wazungu nchini Zimbabwe, na mara nyingi nyimbo zake zilikuwa na ujumbe kwa jamii. Ujumbe huo ulijumuisha ushauri kuhusu virusi vya ukimwi, na nyimbo zake pia zilikuwa na ujumbe ficho ulio kosoa serikali, hatua iliyo sababisha baadhi ya nyimbo zake kupigwa marufuku nchini humo.
Tuku alikuwa muimbaji na mpigaji gita aliye changanya aina tofauti ya miziki, naku unda aina ya muziki iliyo julikana kama Afro-jazz na mashabiki wengi wa muziki wake wali ita aina hiyo ya muziki, "Tuku Music".
Katika safari yake ndefu kimziki, Tuku alitoa albamu 67 naku fanya ziara duniani kote, Australia ikijumuishwa ambako alitumbuiza mashabiki wake kwa mara ya mwisho mwaka wa 2015.

Mfalme wa Afro-Jazz Oliver Mtukudzi, kwenye tamasha Source: EPA
Oliver Mtukudzi, atakumbukwa kwa wimbo wake maarufu kwa jina la Neria, ambao ulitetea usawa wa jinsia.
Share

