Rais wa Kenya Dkt William S Ruto, akiwa pamoja na Dkt Oburu Odinga (kakake Raila) alitoa hotuba fupi aki tangaza rasmi kifo cha Kinara wa chama cha upinzani cha ODM Raila Odinga ambaye anajulikana pia kama "Baba."
Kwa mujibu wa maelezo ya daktari aliye mhudumia Baba, kilicho sababisha kifo chake ilikuwa ni mshutuko wa moyo aliopata alipokuwa akitembea ndani ya pango aliko kuwa akipata huduma ya afya nchini India.
Mwili wa Baba unarejeshwa nchini Kenya ukisindikizwa na baadhi ya viongozi wakiwemo Kiongozi wa Mawaziri wa Kenya Musalia Mudavadi, na Katibu Mkuu wa ODM, Edwin Sifuna miongoni mwa viongozi wengine.
Mwendazake alikuwa ameomba azikwe ndani ya masaa 72 baada ya kuaga dunia, ila kwakuwa mauti yalimkuta nje ya nchi pamoja na taratibu za maandalizi ya mazishi, serikali imetangaza kuwa Baba pewa pumziko la mwisho Jumapili kando ya kaburi la mamake.
Tuta waletea taarifa zaidi punde tutakapo zipokea.

