Ndege hiyo ilikuwa ikitumika kwa safari fupi za ndani ya nchi hiyo ambapo, ilianguka umbali mdogo kabla haijatua katika mji wa Yasuj kusini mwa Irani takribani kilomita 780 toka mji mkuu wa Tehran ambako ilipoanzia kuruka.
Msemaji wa shirika hilo la ndege aina ya Aseman Bwana Mohammad Taghi Tabatabai aliiambia runinga ya taifa kuwa, waliokuwa kwenye ndege namba EP3704 wore wamefariki.
Alisema, ndege hilo ilibeba abiria 59 na pamoja na wafanyakazi wa ndege 6 hivyo kufanya idadi kuwa 65 waliopoteza maisha.
Share

