Watch FIFA World Cup 2026™

LIVE, FREE and EXCLUSIVE

Jahazi la Kimarekani, Comanche, langa'ra

Jahazi la Marekani maarufu kwa jina la Comanche, limepata heshima kubwa kwa kumaliza ungwe ya kwanza ya mashindano ya mashua ya 71 yaanziayo Sydney hadi Hobart. Ni kwa mara ya kwanza, kwa mshindani wa Kimataifa kufanikiwa kuvuka mstari wa heshima baada ya miongo kadhaa kupita.

yatch race
Source: AAP

Jahazi la Marekani maarufu kwa jina la Comanche, imepata heshima kubwa kwa kumaliza ungwe ya kwanza ya mashindano ya mashua ya 71 yaanziayo Sydney hadi Hobart.

Ni kwa mara ya kwanza, kwa mshindani wa Kimataifa kufanikiwa kuvuka mstari wa heshima baada ya miongo kadhaa kupita.

Upepo hafifu kwenye kingo za mto Derwent pia ulichangia kuchelewa muda wa kumaliza wa siku mbili, masaa 9, dakika 58 na sekunde 30.

Mashua hiyo ilionyesha ubora wake wa kujikimu baada ya kukumbwa na misukosuko kutokana na kuchafuka kwa bahari iliyoifanya mashua hiyo kuonekana kupoteza kipande cha ubao kusaidia usawa wa mashua na kile kipande cha ubao cha kuongozea.

Nahodha wa Marekani wa mashua ya 'super-maxi', Bwana Ken Read, amesema, ilikuwa almanusra watangaze kutoendelea na mashindano.

Alisema; "Hivyo, wakati tunasema oh, tumemaliza na tumesimama na tukashusha matanga yote chini, na baadaye tukaanza kama kuendesha kurudi kurejea Sydney na ndipo ghafla nikaona chombo walichokuja nacho hawa watu, hiyo huwa daima ni alama nzuri kwamba wao wana upeo."

Kwa sasa basi mashua ya Comanche imeshajichukulia mstari wa heshima, kipaumbele kimegeukia kwa nani kuchukua ushindi wa jumla wa heshima.

Comanche bado inaendelea na mashindano ili kushinda mistari yote ya kumalizia na ushindi wa Jumla.


2 min read

Published

By Frank Mtao

Source: SBS News



Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Stream now