Amonde: 'Hatu ogopi timu yoyote'

Timu ya raga ya taifa ya Kenya ya wachezaji saba (Shujaa) imewasili mjini Sydney ikiwa na matumaini mengi.

Andrew Amonde nahodha wa timu ya taifa ya Kenya, ya raga ya wachezaji saba

Andrew Amonde nahodha wa timu ya taifa ya Kenya, ya raga ya wachezaji saba azungumza na SBS Swahili Source: Picha: SBS Swahili

Shujaa wamewasili mjini Sydney baada yakuwapa Blitz Bokke wa Afrika Kusini kichapo ambacho hawaku tarajia mjini Hamilton New Zealand.

Nahodha wa Shujaa Andrew Amonde alipo zungumza na SBS Swahili alisema kwamba: "Tuko katika kundi gumu lakini tumejiandaa ipaswavyo, na wachezaji wetu wako tayari kushindana na timu yoyote katika michuano ya Sydney 7s. Tuna waomba mashabiki waje kwa wingi, sababu support yao ni muhimu sana kwetu."

Bila shaka Shujaa wamejipata katika kundi gumu sana ambalo lina jumuisha, Wales, Fiji na New Zealand. Mechi ya kwanza ya Shujaa itakuwa dhidi ya Fiji tarehe 1 Februari 2020, saa nane na dakika tisa, katika uwanja wa Bankwest Stadium, mjini Parramatta NSW.

SBS Swahili itakupa matokeo yote ya mechi za shujaa kupitia mitandao yetu yakijamii na katika tovuti hii.


Share

Published

By Gode Migerano
Presented by Gode Migerano
Source: SBS Swahili

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Amonde: 'Hatu ogopi timu yoyote' | SBS Swahili