Waziri Mkuu Scott Morrison, alihotubia taifa usiku wa Jumamosi 21 Mei 2022 nakutoa shukrani zake za dhati kwa taifa na washiriki wake kwa muda alio ongoza nchi.
Katika hotuba yake Bw Morrison alisema pia kuwa alikuwa amezungumza na kiongozi wa upinzani Bw Albanese nakumpongeza kwa kushinda uchaguzi mkuu. Licha yakuwa hesabu za kura bado zina endelea, hakuna uwezekano wa chama cha mseto kuweza kuunda serikali.
Bw Anthony Albanese alishukuru taifa kwa kumpa heshima yakuongoza taifa, pamoja nakumshukuru mtangulizi wake Bw Morrison kwa huduma aliyotoa kwa taifa. SBS Swahili itachapisha matokeo kamili ya uchaguzi mkuu, punde tutakapo yapata.