Takribani watu 47 wamefariki baada ya mabasi mawili kugongana uso kwa uso Kaskazini-Mashariki nchini Zimbabwe, kituo cha runinga ya taifa kilieleza.
Ajali hiyo ilitokea siku ya Jumatano karibu na mji wa Rusape, kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Zimbabwe.
Miongoni mwa waliofariki ni watu wazima 45 na watoto wawili, alikaririwa akisema msemaji wa polisi Paul Nyathi.
Mabasi hayo yalikuwa yakisafiri kati ya mji mkuu Harare, na mji wa Mutare.
Kama ilivyo kwa mataifa mengi ya Afrika, ajali za barabarani zimekuwa za kawaida nchini Zimbabwe kutokana na miundo mbinu mibovu ya barabara na uhaba wa magari ya uhakika.
Tutawaletea habari zaidi.
Share

