Kikundi cha Kiislamu wenye msimamo mkali wamelipua bomu la kujitoa mhanga kwa kutumia gari karibu na jumba la rais kwenye mji mkuu wa Somalia Mogadishu, na kuua angalau watu tisa, ikiwa ni pamoja na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Hussein Elabe Fahiye.
Kapteni Mohamed Hussein aliwaambia waandishi wa habari kuwa, watu 13 walijeruhiwa na majeruhi wengi walikuwa askari.
Kikundi cha kigaidi cha al-Shabab cha Somalia, kilidai kuhusika na mlipuko huo, kikisema kuwa kililenga kushambulia magari yaliobeba viongozi wa serikali.