Mpango wa makubaliano ya kibiashara baina ya Indonesia na Australia, utasainiwa wiki ijayo, taarifa kutoka Jakarta zilisema, baada ya miezi ya mvutano wa kidiplomasia juu ya mpango wa Canberra kuhamisha ubalozi wake kwenda Yerusalemu.
Waziri wa biashara wa Indonesian Enggartiasto Lukita na mwenzake wa Australia Simon Birmingham wako tayari kusaini makubaliano ya dola bilioni kadhaa mjini Jakarta Jsiku ya umatatu, kulingana na mwaliko wa wizara ya biashara waliotuma kwa waandishi wa habari.
Mkataba huo utajumuisha upatikanaji bora wa mifugo kama vile ng'ombe na kodoo kwa watu milioni 260 wa Indonesia, wakati vyuo vikuu vya Australia, watoa huduma za afya na wachimbaji madini pia watafaidika kwa pande zote mbili za kiuchumi mkubwa zaidi wa mashariki kusini mwa Asia.
Ufikiaji mkubwa wa soko la Australia unatarajiwa kuwezesha viwanda vya magari na nguo vya Indonesia, na kuongeza mauzo ya mbao, vifaa vya umeme na dawa.

Trade Minister Simon Birmingham is in Indonesia to sign the long-awaited free trade deal. Source: AAP
Biashara ya nchi hizi mbili ziliingiza dola bilioni 16.3 mwaka 2017.
Mpango huu umekuwa katika mazungumzo tangu mwaka 2010 na ulitarajiwa kutiwa saini kabla ya mwisho wa mwaka jana lakini ulisimama wakati Waziri Mkuu Scott Morrison alipopendekeza kuhamishwa kwa ubalozi wa Australia huko Yerusalemu.

Australia's Prime Minister Scott Morrison and Indonesia's President Joko Widodo at a bilateral meeting during the 2018 ASEAN Summit in Singapore. Source: AAP
Mr Morrison mwanzoni alielezea mabadiliko hayo kwenye mwezi Oktoba, ikiwa ni kabla ya uchaguzi muhimu wa Wentworth, ambao huwa na idadi kubwa ya Wayahudi. Indonesia, taifa la Waislamu wengi ulimwenguni, lilikasirika na pendekezo hilo.
Share

