Katika muda huo, Australia ilicheza dhidi ya timu ya Falme zakiarabu nakuibuka mshindi kwa magoli mbili kwa moja nakusogea hatua mbele kushiriki katika mechi dhidi ya Peru itakayo amua timu ya mwisho itakayo shiriki katika kombe la dunia baadae mwaka huu.
Alfajiri ya leo 14 Juni 2022, Australia ili ingia dimbani dhidi ya Peru katika mechi iliyo kuwa na nafasi chache kwa timu zote kufunga goli. Dakika za kwanza tisini ziliisha bila mshindi, na katika dakika za nyongeza hazikutosha kwa pande yoyote kupata ushindi hatua iliyo salia ilikuwa penati kuamua mshindi.
Australia ili ibuka mshindi wa magoli tano kwa nne dhidi ya Peru, nakujikatia tiketi yakucheza katika kombe la dunia nchini Qatar.