Australia ili ingia uwanjani dhidi ya Denmark ikijua lazima ishinde mechi yake la sivyo ushiriki wao katika Kombe la Dunia utakuwa mashakani.
Kama ilivyo tarajiwa nakutabiriwa, Denmark ilimiliki mpira kwa muda mrefu, ila hiyo yote haikutosha kutikisa walinzi wa Australia katika mechi hiyo. Na katika dakika ya 60, nyota wa Melbourne City FC, Mathew Leckie aliwakwepa walinzi wa Denmark nakufyatua kombora kwa mguu wake wakushoto hadi ndani ya wavu wa Denmark.

Wakati huo huo katika mechi nyingine yakundi lao, Tunisia walikuwa wakiwapa matatizo bingwa watetezi Ufaransa na licha yakushinda mechi hiyo, ushindi wa Australia ulikuwa na maana kwamba Denmark pamoja na Tunisia walitupwa nje ya michuano hiyo.
Australia sasa inajiandaa kukabiliana na mtihani mgumu kutoka Lionel Messi na Argentina alfajiri ya Jumapili kwa masaa yamashariki Australia.

