Bwana Ricketson mwenye umri wa miaka 68, ataendelea kusubiri hadi tarehe 31 mwezi huu pale ombi lake la dhamana yake kusikilizwa tena na Mahakama Kuu ya Cambodia.
Maafisa nchini Cambodia, wanamchunguza Bwana Ricketson kwa madai ya kujihusisha na chama cha upinzani kilichofutwa ambacho kilituhumiwa kwa hujuma za kumuangusha Waziri Mkuu wa nchi hiyo bwana Hun Sen.
Mnamo mwezi wa sita, Bwana Ricketson alikamatwa kwa tuhuma hizo baada ya kandege kadogo kakuchukulia picha na video 'drone' kurushwa hewani juu ya maandamano ya kisiasa ambapo kilikuwa kikinasa matukio yote.
Alitupwa jela ngumu ya Prey Sar katika mji mkuu wa Cambodia, Phnom Penh.
Bwana Ricketson ambaye ameshasafiri nchini humo mara kwa mara katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, alikuwa akitengeneza filamu kuhusu jamii zinavyoishi katika hali duni kwenye eneo la takataka nyingi nchini humo, kwa mujibu wa shirika la habari la Channel 9.
Inasemekana, utawala wa sasa wa Bwana Hun Sen ni mkali zaidi kulinganisha na awali na hii ni kabla ya uchaguzi wa mwezi wa saba mbapo anatarajiwa kuongeza zaidi muhula wa utawala baada ya huu wa miaka 32 aliyonayo madarakani kwani hadi sasa amekwisha muondoa mpinzani wake na kupelekea pia kukivunjilia mbali chama kikuu cha upinzani mwezi wa kumi na moja, kitendo kinachopigiwa kelele na wana demokrasia wa magharibi.
Bwana Rickets amenukuliwa akisema, ana matumaini serikali ya Australia itatetea haki yake ya kujieleza kwani kwa mujibu wa katiba ya Cambodia, inamthibitisha kuwa na haki ya kujieleza.
Share

