Mabalozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa waliokuwa wakishiriki katika kikao hicho, walikemea vikali maamuzi ya serikali ya Ukraine kuzindua shambulizi hilo, hata hivyo balozi wa Urusi alitetea serikali yake kwakusema wanacho fanya ni oparesheni maalum yakijeshi nasi uvamizi wa Ukraine.

Raia wakimbia kutoka nyumba iliyo gongwa kwa shambulizi la anga katika kijiji cha Luhanskaya, Ukraine. Source: World Press Photo
Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison na Kiongozi wa Upinzani Anthony Albanese kwa sauti moja wamekemea shambulizi hilo la Urusi, na Waziri Mkuu ametangaza vikwazo vya ziada vinavyo walenga wandani wa serikali ya Urusi. Imeripotiwa kuwa takriban idadi ya watu 50 wame fariki, na mamia kujeruhiwa katika siku ya kwanza ya uvamizi huo, ila idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka. Raia wa Australia wenye asili ya Ukraine wamefanya maandamano kote nchini, kupinga uvamizi wa Urusi.