Baada ya pande zote kuwasilisha kesi zao na mahakimu kujadiliana kwa upana, Hakimu Mkuu Maraga alisoma uamuzi wa mahakimu wenza.
Hakimu Mkuu Maraga alieleza mahakama na taifa kwamba, uamuzi ulifikiwa kwa wingi wa mahakimu wanne ilhali wawili walipinga uamuzi huo. Hata hivyo matokeo yaliyo mpa rais Uhuru Kenyatta ushindi dhidi ya Raila Odinga yame futwa na uchaguzi mpya kuamuriwa kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya.

Mahakimu ndani ya mahakama kuu, Nairobi, Kenya Source: Nairobi News
Licha ya kuto toa maelezo kwa upana ya uamuzi huo, hakimu mkuu Maraga ame amuru tume ya uchaguzi IEBC, kuandaa uchaguzi mpya wa urais.
Share

