Maandalizi ya miezi sita ya msimu mpya wa A-League yali malizwa katika uwanja wa AAIMI mjini Melbourne, mshambuliaji wa Melbourne City Bruce Kamau alipo chukua sheria mkononi katika dakika za mwisho wa kipindi cha kwanza katika mechi ya kwanza ya msimu dhidi ya Brisbane Roar.
Bruce Kamau alipokea mpira nje ya eneo la hatari, nakufyiatua mkwaju mkali na mpira huo ulitikisa wavu licha ya juhudi za mlinzi wa Brisbane Roar kujaribu kuuzuia kuingia wavuni.
Kamau alihakikisha ushindi wa Melbourne City katika dakikta ya 75 alipo fyatua mkwaju mwingine ambao ulimgonga mlinzi wa Brisbane Roar naku salia wavuni kwa mara ya pili. Goli hilo lilimpa Bruce Kamau tuzo ya mchezaji bora katika mechi yaku fungua msimu mpya wa 2017/18 A-League.
Share

