Katika ujumbe wa Twitter, msemaji wa serikali ya Burundi Balozi Willy Nyamitwe alitangaza kuwa Rais Peter Nkurunziza amefariki baada yakukabiliwa na mshtuko wa moyo.
Rais Nkurunziza aliongoza Burundi kwa miaka 15 na alikuwa aondoke madarakani miezi michache ijayo baada, ya Generali mstaafu Evariste Ndayishimiye kushinda uchaguzi wa rais siku chache zilizo pita.