Licha ya Australia kuanza mechi kwa kasi dhidi yawa Syria, wageni ndio walio funga goli ya kwanza katika dimba hilo. Kosa la Mark Milligan katikati ya uwanja lili adhibiwa kwa mkwaju wa Omar Al Soma wa Syria aliye funga goli la kwanza la mechi hiyo.
Socceroos wali endelea kushambulia lango la Syrian na hatimae suluhu iliwasili kupitia krosi ya Matthew Leckie, ambayo ilipokewa kwa furaha na Tim Cahill, ambaye hakusita kuuvunja moyo wa mlinda lango la Syria kwaku funga goli kwa kichwa.
Mechi hiyo ilikamilika kwa sare ya 1-1 na punde baada ya mechi kuanza katika dakika 30 za nyongeza, mzigo wa Socceroos uliregezwa baada ya mchezaji wa Syria, Mahmoud Al Maowas kuonesha kadi nyekundu nakuondolewa uwanjani.
Mshindi wa mechi hiyo aliamuliwa katika kipindi cha pili cha dakika 30 za nyongeza, kupitia goli la pili la Tim Cahill katika dakika ya 106. Ila kabla ya mwamuzi kupuliza kipenga cha mwisho, matumaini ya Australia na Syria yalisalia katika miguu ya Omar Al Soma katika dakika ya 120 aliye pewa fursa yaku chambua kitendawili hicho.
Hesabu ilikuwa rahisi, akifunga goli Syria itaendelea katika hatua ya mwisho yakufuzu na Australia ina aga michuano hiyo, ila asipo funga goli hilo basi Syria ndiyo ita aga michuano hiyo. Mamilioni yama shabiki kutoka pande zote walipokuwa wakimwomba Maulana aingilie kati, mkwaju wa Omar Al Soma aligonga mwamba nakuzua shangwe na vigelegele toka kwa mashabiki wa Socceroos, wakati mashabiki wa Syria walisalia na maswali chungu nzima.
Australia sasa ita subiri kujua ni nani kati ya Panama au Honduras atakaye menyana naye, katika hatua ya mwisho yakufuzu kwa kombe la dunia nchini Urusi.
Share

