Feature

Chris Minns a ahidi 'mwanzo mpya' kwa NSW Labor inapo elekea kuunda serikali ya wengi

Chama cha Labor sasa kina ongoza kote nchini Australia, baada ya jimbo la mwisho ambalo chama cha mseto kilikuwa kina ongoza kushindwa katika uchaguzi.

A man and a woman celebrating

Labor leader and Premier-elect Chris Minns, čelnik Laburističke stranke i novoizabrani premijer Novog Južnog Walesa sa suprugom Annom na proslavi izbornih rezultata Source: AAP / Dean Lewins

Key Points
  • Mr Perrottet conceded defeat in a phone call to Mr Minns about 9pm on Saturday.
  • Labor is tipped to gain the 47 seats it needs to govern in its own right.
  • Both leaders have campaigned hard in vital seats in Sydney's west, where a third of NSW voters live.
Uongozi wa serikali za Labor katika sehemu zote za bara la Australia umekamilika, Tasmania ndilo jimbo pekee ambalo liko chini ya uongozi wa serikali ya chama cha Liberal.

Kulingana na hesabu za kura zinazo endelea kutoka uchaguzi wa Jumamosi, Chris Minns amekuwa kiongozi mpya wa NSW na anatarajiwa kuongoza serikali ya wengi ya chama cha Labor.

Katika hotuba yake ya ushindi, kiongozi mteule wa jimbo alitangaza kuwa chama chake "kimerejea nakiko tayari kuongoza".

"Hatuta waangusha watu wa jimbo hili," Bw Minns alisema.

"Tuta ongoza kwa kila mtu jimboni NSW. Tunajua kuwa changamoto ni kubwa na majukumu ni makubwa ila, NSW Labor imerudi na iko tayari kuongoza katika jimbo hili mhimu."

Bw Minns alimshukuru pia kiongozi wa Liberal anaye ondoka madarakani Dominic Perrottet kwa huduma yake.

"Hakuna shaka kampeni ya uchaguzi huu ilikuwa yakipekee, mfano wa heshima na ustaarabu. Hakuna chama kilicho fanya kampeni hasi," alisema.
Waziri Mkuu Anthony Albanese alihusika pakubwa katika siku ya uchaguzi katika maeneo kadhaa ya Sydney, na alimkaribisha Bw Minns kwenye jukwaa la ushindi mjini Sydney kutoa hotuba yake.

"Anawakilisha kila kitu kilicho bora kuhusu chama cha Labor cha Australia," Waziri Mkuu alisema kumhusu Bw Minns.

"Moano yake ni yale ambayo huwa yanawajumuisha watu moyoni mwake."

Bw Albanese alitaja uadilifu, maono na usawa kuwa ni miongoni mwa sifa zinazo mwongoza.
Ushiriki wa Bw Albanese kando ya Bw Minns mara kadhaa katika kampeni za uchaguzi wa jimbo la NSW, ulikuwa tofauti na jinsi kiongozi wa upinzani wa mseto Peter Dutton alivyo kosekana katika kampeni za chama cha mseto ambacho kilikuwa kina jaribu kusalia madarakani.

Katika ukimbi wa sherehe za chama cha Labor, waziri wa shirikisho Chris Bowen alisema Bw Mr Minns "aliongoza kampeni nzuri sana".

"Anaweza kuwa kiongozi mhimu wa Labor kama (Neville) Wran na (Bob) Carr," ali eleza waandishi wa habari.

Perrottet atoa pendekezo

Katika mazungumzo kwa simu na Bw Minns mida ya saa tatu usiku wa Jumamosi, Bw Perrottet alikiri kushindwa.

Kiongozi anaye ondoka madarakani, alihamasisha NSW isimame kidete na Bw Minns kwa maslahi ya nchi.

"Naomba kila mtu kote NSW, bila kujali upande wa siasa unao penda, muunge mkono kwa sababu, NSW inapofanya vizuri, nchi yetu itafanya vizuri pia na, hicho ni kitu na amini sote tunaweza ungana kuhusu."

Bw Perrottet, aliyekuwa kiongozi wa NSW miezi 18 iliyopita baada ya kiongozi wa jimbo hilo Gladys Berejiklian kujiuzulu katikati ya uchunguzi wa ufisadi, na alikuwa akiwania awamu ya nne kwa niaba ya serikali ya mseto.

Bw Perrottet alisema kuwa Bw Minns atakuwa kiongozi mzuri mbadala, pamoja nakuchua wajibu kamili kwa matokeo ya chama chake katika uchaguzi huo.

"Na ndio, matokeo hayo yana maana kwamba nita jiuzulu kutoka uongozi wa chama cha Liberal bungeni."

"Ni wazi kabisa tunahitaji mwanzo mpya."

Tathmini kwa Liberals

Ndoto ya chama cha Labor ilipokuwa ikitimia, uchambuzi wa jinsi chama cha Liberal kilivyo shindwa ulikuwa ukianza.

Waziri Mkuu wa zamani na kiongozi wa chama cha Liberal John Howard aliwasili katika ukumbe wa uchaguzi wa chama chake, akisita kuzungumza kuhusu matokeo ya uchaguzi akisema "ni mapema sana kuzungumzia hoja hiyo".

Alisema kuwa Dominic Perrottet alikuchukua kazi ya uongozi wa chama, "katika mazingiria magumu sana" baada ya kuondoka ghafla madarakani kwa Gladys Berejiklian.

"Ana nishangaza sana," Bw Howard alisema kuhusu kiongozi wa NSW anaye ondoka madarakani.

Punde baadae alipokea taarifa kuhusu mpango wa Bw Perrottet kujiuzulu kama kiongozi wa chama cha Liberal.
Msemaji wa hazina wa shirikisho wa chama cha Liberal Angus Taylor, aliulizwa kama sera endelevu za chama cha Liberal kuhusu mabadiliko ya mazingira pamoja na kura za mji, zilichangia kwa chama hicho kupoteza kura katika maeneo ya vijijini.

"Lazima ufanye kampeni katika ngome zako," Bw Taylor alieleza shirika la habari la Sky.
NSW STATE ELECTION
NSW Premier Dominic Perrottet with his wife Helen Perrottet and daughter Celeste arrive to cast their votes on NSW state election day. Source: AAP / AAP
Viongozi wote wawili walifanya kampeni katika maeneo bunge mhimu ya Magharibi Sydney, ambako theluthi tatu yawapiga kura wa NSW wanaishi, na maeneo bunge mengi yako katika hali tete.

Kiongozi wa jimbo alipiga kura katika kitongoji cha Beecroft Jumamosi akiwa pamoja na mkewe na bintiye Celeste, wakati watu wakujitolea katika shule walikuwa waki uza keki na sausage kwa wapiga kura.

Bw Minns alipiga kura katika eneo bunge la kusini Sydney la Kogorah ambalo lina ushindani mkubwa, akiwa pamoja na mkewe Anna pamoja na watoto wake watatu wakiume, na aliahidi jimbo lake maono mapya.

"Piga kura kwa mwanzo mpya wa NSW, kwa timu yenye mpango kwa huduma mhimu, kwa shule zetu na kwa hospitali zetu, atakaye simama dhidi ya ubinafsishaji pamoja nakuwa wake watu wa NSW kanza," alisema.
NSW STATE ELECTION
NSW Premier Dominic Perrottet (far left) and his wife Helen Perrottet (second left) voting on NSW state election day, in the seat of Epping, in Sydney, Saturday, March 25, 2023. Source: AAP / AAP
Dai Li ni mbunge huru wa shirikisho wa Fowler, amedokeza kulikuwa mchoko kwa masharti magumu ya vizuizi vya UVIKO-19 ambavyo vili athiri jamii yake ya Sydney wakati wa uongozi wa serikali ya mseto ya NSW.

"Wakati huo tulikuwa tukizungumza kama raia wasio na thamani. Nadhani bado kuna mabaki ya hali hiyo katika jamii yetu na, kwa hiyo kuna hisia kuwa tulipuuzwa na serikali," ali eleza shirika la habari la ABC.

Share

Published

Presented by Gode Migerano
Source: AAP

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service