Sherehe hizo za ufunguzi kwa michuano ya Jumuiya za Madola Gold Coast , inafanyika katika uwanja wa Carrara, kukiwa na watumbuizaji takribani 4,000 wanaowatumbuiza wanariadha na mashabiki.
Sherehe hizo za maisha ya pwani kama Dhahabu kwa Gold Coast na tamaduni za Waustralia wa Aborigino, imekuwa ndio alama kubwa ya sherehe hizo.
Umati wa mashabiki 35,000 waliojitokeza katika uwanja huo, wanaburudishwa na wasanii kama Christine Anu, Ricki-Lee Coulter na Delta Goodrem, ambapo Mfalme wa Wales, charles amezindua ramsi michuano hiyo inayoanza leo tare 4 hadi 15 mwezi huu wa nne.
Wakati hayo yanaendelea, wa Aborigino wamekuwa wakitumia mwanya wa michuano hiyo kuandamana kupinga historia ya uvamizi wa Australia.
Share

