Hatu hiyo imejiri wakati wafuasi wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance (NASA), wanaendelea kuwasili katika bustani ya Uhuru ambako vinara Raila Odinga na naibu wake Kalonzo Musyoka wata apishwa.

Wafuasi wa NASA wampa Biblia kinara wao Raila Odinga kwa ajili yaku apishwa Source: NASA Kenya
Taarifa zilikuwa zimesambaa katika vyombo vya habari na mtandaoni kuhusu onyo toka kwa serikali kwa wawakilishi wa vyombo vya habari nchini humo ambao walikuwa wame alikwa kwa mkutano maalum ndani ya ikulu mjini Nairobi. Imeripotiwa kuwa serikali ilionya vyombo vya habari dhidi yakupeperusha picha na matangazo ya moja kwa moja ya hafla hiyo ya uapisho. Kufungwa kwa matangazo ya vyombo hivyo vya habari kuna zungumziwa mjini Nairobi, kama adhabu ya serikali kwa vyombo hivyo vya habari ambavyo havija tii amri ya serikali. Image
Chama cha wahariri wa habari nchini Kenya kimekosoa amri ya Ikulu yakuto peperusha picha za hafla ya uapisho wa upinzani.
SBS Swahili ita endelea kukupasha taarifa ya matukio ya uapisho wa vinara wa upinzani kutoka bustani ya Uhuru mjini Nairobi, punde tutakapo pata taarifa hizo.
Share

