Taarifa mpya ya COVID-19: ACT yaongeza muda wa makatazo, na mamlaka waomba watu wachukue chanjo za AstraZeneca

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 31 Agosti 2021.

The ACT reported 13 new local COVID-19 cases on Tuesday, including at least eight that were infectious in the community.

The ACT reported 13 new local COVID-19 cases on Tuesday, including at least eight that were infectious in the community. Source: AAP Image/Lukas Coch

  • Jimboni NSW, 67% yawakaaji wamepokea dozi yao ya kwanza ya chanjo
  • Jimbo la Victoria lina zaidi ya maeneo 1,000 ya maambukizi ya COVID-19
  • Wilaya ya ACT imeongeza muda wa makatazo hadi 17 September
  • Jimbo la SA lainua vizuizi kwa wasafiri kutoka Wilaya ya Kaskazini na Queensland

New South Wales

NSW imerekodi kesi mpya 1,164 zamaambukizi ndani ya jamii, kesi 796 zikiwa katika maeneo ya Magharibi na Kusini Magharibi Sydney. Watu watatu walifariki. 

Afisa Mkuu wa Afya wa jimbo hilo Dr Kerry Chant ame wahamasisha wakaaji wa vitongoji vya Guildford, Merrylands, Auburn, Greenacre, Bankstown na Blacktown wakapimwe.

Waziri wa Afya wa NSW Brad Hazzard ame shauri mtu yeyote ambaye ana zaidi ya miaka 18, apate chanjo ya AstraZeneca kwa sababu hakuna chanjo zakutosha za Pfizer. 

Mwanaume mmoja waki Aboriginal mjini Dubbo, alitangazwa Jumatatu kama mtu wakwanza kufa, kwa sababu ya COVID-19 katika mlipuko wa sasa katika eneo la Magharibi ya New South Wales.

Bonyeza hapa kufanya miadi yako ya chanjo ya COVID-19 leo.

Victoria

Victoria imerekodi kesi mpya 76 ndani ya jamii, zikijumuisha kesi 31ambazo bado hazija ungwa na milipuko ya sasa. 

Kiongozi wa jimbo hilo Andrews, ambaye ata tangaza mpango wakuregeza vizuizi kesho, amesema 'chanjo sahihi ni ile ambayo unaweza pata', akidokeza kuhusu upatikanaji kwa wingi wa dozi za chanjo za AstraZeneca.

Kwa sasa kuna zaidi ya sehemu 1,000 kwenye orodha ya sehemu za maambukizi, ikijumuisha majengo kadhaa mjini Melbourne.

Pata hapa kituo cha chanjo kilicho karibu yako.

Australian Capital Territory

Wilaya ya The ACT imerekodi kesi mpya 13 ndani ya jamii, angalau kesi nane zikiwa zilikuwa ndani ya jamii zilipokuwa katika hali ambukizi. 

Zahanati ya watu wengi ya chanjo za COVID-19 mjini Canberra, itafunguliwa katika ukumbi wa Taasisi ya Michezo ya Australia Ijumaa, 3 Septemba. Muda wa makatazo ume ongezwa hadi 17 Septemba, vizuizi vipya vikiwepo kuanzia saa 11 jioni ya Alhamisi.   

Tazama ustahiki wako kwa chanjo za COVID-19 hapa.

Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
  • Kusini Australia yainua vizuizi vyote kwa watu wanao safiri kutoka Kusini Mashariki Queensland na Katherine katika Wilaya ya Kaskazini.
alc covid mental health
Source: ALC

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

NSW Safari & usafiri na Karantini

VIC Vibali vya safariWasafiri wa ng'ambo na Karantini

ACT Usafiri na Karantini

NT Safari na Karantini

QLD Safari na Karantini

SA Safari na Karantini

TAS Safari na Karantini

WA Safari na Karantini

Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:

COVID-19 Vaccination Glossary
Appointment Reminder Tool.


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania

Northern Territory 


Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania
Northern Territory

 


Share

3 min read

Published

By SBS/ALC Content

Presented by Gode Migerano

Source: SBS




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now