- Australia imerudisha nyuma ratiba yakufungua mipaka yakimataifa kwa watu wenye viza za ujuzi, wanafunzi pamoja na watu wenye viza zakibinadam, watu wenye viza zakufanya kazi wakiwa likizoni pamoja na watu wenye viza za familia kuanzia 1 Disemba hadi 15 Disemba.
- Waziri wa Shirikisho wa Afya Greg Hunt amesema ushauri waki Afya utaongoza mageuzi yoyote ya usoni kwa hatua hiyo.
- Upinzani wa shirikisho ume unga mkono uamuzi wa serikali, wakusogeza mbele hatua yakufungua mipaka yakimataifa.
- Baraza lamawaziri lakitaifa limeratibiwa kukutana leo, kujadili majibu yakitaifa, jimbo na wilaya kwa tisho la aina mpya ya kirusi cha Omicron wakati naibu afisa mkuu wa afya amesema maambukizi ya kirusi hicho yamo ndani ya jamii.
- Kuna kesi sita ambazo zime thibitishwa za aina ya kirusi cha Omicron, ambazo ziko ndani ya karantini nchini Australia.
- Jimbo la Magharibi Australia linakaribia kufikia tarehe ya mwisho kwa utoaji wa chanjo wa lazima kwa sekta kadhaa.
- Queensland ime amuru wafanyakazi katika sekta zinazo zingatiwa kuwa zenye hatari kubwa wapate chanjo kuanzia 17 Disemba.
TAKWIMU ZA UVIKO-19:
Victoria imerekodi kesi mpya 918 ndani ya jamii pamoja na vifo sita.
NSW imerekodi kesi mpya 179 ndani ya jamii pamoja na vifo vitatu.
Karantini na vizuizi jimbo kwa jimbo:
Usafiri
Msaada wa fedha
Kuna mageuzi kwa malipo ya janga ya UVIKO-19, punde majimbo yanapo fikisha lengo la 70% na 80% ya watu ambao wame pata chanjo kamili: Kupata msaada wakati wa UVIKO-19 kutoka shirika la Services Australia katika lugha yako
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60 sbs.com.au/coronavirus
- Pata hapa miongozo inayofaa kwa jimbo lako au wilaya yako: NSW, Victoria, Queensland, Western Australia, South Australia, Northern Territory, ACT, Tasmania.
- Pata hapa taarifa kuhusu chanjo ya UVIKO-19 katika lugha yako.
Tazama rasilimali zilizo tafsiriwa nakuchapishwa na Huduma ya Mawasiliano ya Afya ya Tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya: