Taarifa mpya kuhusu UVIKO-19: Australia yarekodi vifo 25 katika majimbo tano

Hii ni taarifa yako mpya kuhusu UVIKO-19 nchini Australia kwa Machi 22.

Watu wavuka barabara mjini Melbourne

Watu wavuka barabara mjini Melbourne Source: AAP

  • Victoria imerekodi vifo vipya visaba vya UVIKO-19, wakati watu wanne walikufa kwa sababu za virusi hivyo NSW na Kusini Australia. 
  • Queensland imerekodi vifo vingine vinne, wakati Tasmania imeripoti kifo kimoja.
  • Naibu Afisa Mkuu wa Afya wa NSW Marianne Gale, amewahamasisha wazazi wa watoto wenye miaka tano na zaidi, wa hakikishe wana chanjwa 'bila kuchelewa', akiongezea kuwa watoto wengi kwa sasa wana fuzu kupokea dozi yao ya pili.
  • Serikali ya jimbo la Victoria imetangaza kuwa vocha 140,000 za safari, zitatolewa kwa umma kuanzia saa 8 mchana Jumatano.
  • Mfumo huo unawapa wanao wasilisha maombi marejesho ya $200, wakitumia zaidi ya $400 kwa makazi au sehemu zingine zakitalii.
  • Kiongozi mteule wa Kusini Australia Peter Malinauskas, ameweka wazi mfumo mpya wa serikali ambao amesema, unaonesha jimbo hilo linaweza fikisha kesi mpya 8,000 za maambukizi ya kila siku ya UVIKO-19 kufikia Aprili.
  • Maafisa wa afya wa SA waliweka tena ila hawakutangaza, marufuku kwa baadhi ya upasuaji wakuchagua katika hospitali za umma, siku moja kabla ya uchaguzi wa jimbo uliofanywa Jumamosi.

Takwimu za UVIKO-19 Australia

New South Wales imeripoti wagonjwa 1,177 wame lazwa hospitalini 41 kati yao wakiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti. Kulikuwa vifo vinne na kesi mpya 20,960 za UVIKO-19.

Jimboni Victoria, watu 256 wame lazwa hospitalini 24 kati yao wakiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti na 5 kati yao wanapumua kwa msaada wa mashine. Kulikuwa vifo saba pamoja na maambukizi mapya 9,594.

Tasmania imerekodi kifo kingine kimoja pamoja na kesi mpya 1,825 za UVIKO-19. Kuna watu 25 ambao wamelazwa hospitalini kwa sababu ya UVIKO-19.

Katika wilaya ya ACT watu 38 wamelazwa hospitalini wakiwa na UVIKO-19, watatu wakihitaji huduma katika kitengo cha wagonjwa mahtuti na idadi ya maambukizi mapya 1,014 yameripotiwa.

Jimboni Queensland, kumeripotiwa kesi mpya 8,881 za maambukizi ya UVIKO-19 pamoja na vifo tisa. watu 252 wame lazwa hospitalini wakiwa na UVIKO-19, na wagonjwa tisa wanahudumiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti.

Na jimbo la Kusini Australia limerekodi vifo vingine vinne pamoja na kesi mpya 3,686 za maambukizi ya UVIKO-19. Kuna watu 165 ambao wame lazwa hospitalini kwa sababu ya virusi hivyo, 11 kati yao wanahudumiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti.


 


 



 

Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19 hapo chini



Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa chini, kama matokoe ya kipimo chako ni chanya 



Jua unacho weza na chenye hauwezi fanya kokote nchini Australia

Kama unahitaji msaada wakifedha, tazama chaguzi zako ni gani




Soma taarifa zote kuhusu UVIKO-19 katika lugha yako kwenye tovuti ya Coronavirus ya SBS.


Share

Published

Updated

Presented by Gode Migerano

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service