Taarifa mpya ya UVIKO-19: Australia yaripoti vifo 42, abiria wapatwa na uviko ndani ya meli yakitalii WA

Hii ni taarifa yako mpya kuhusu UVIKO-19 nchini Australia kwa 26 Aprili 2022.

Western Australia could ease health restrictions this week. (file)

Western Australia could ease health restrictions this week. (file) Source: AAP Image/Richard Wainwright

Australia iliripoti vifo 42 vya UVIKO-19, vifo 18 vikiwa New South Wales na vifo 15 Victoria, Jumanne. Takwimu kutoka Magharibi Australia zilijumuisha vifo saba vya kihistoria.

Tazama mitindo mipya ya kesi za UVIKO-19, kulazwa hospitalini na vifo Australia hapa.


Abiria kumi na wafanyakazi wawili walipatwa na UVIKO-19 ndani ya meli yakitalii Magharibi Australia.

Meli hiyo yakitalii, Coral Discoverer, iliwasili mjini Broome mapema Jumatatu baada ya safari ya siku 10 Jumatatu kutoka Darwin. Abiria wote ndani ya meli hiyo wame pata chanjo tatu za UVIKO.

Magharibi Australia ilikuwa imeruhusu meli ndogo zakitalii, zenye abiria wasio zidi 350 na wafanyakazi, kuingia jimboni humo kuanzia 17 Aprili 2022.

Kuna uwezekano serikali ya Magharibi Australia inaweza futa amri zakuvaa barakoa wiki hii, wakati idadi ya kesi mpya za UVIKO-19 inaendelea kuto ongezeka jimboni humo.

Nancy Baxter, ni mtaalam masomo ya udhibiti wa magonjwa katika Chuo cha Melbourne, ana amini ni mapema sana kuregeza vizuizi wakati New South Wales, Victoria, Australian Capital Territory na Queensland wikijana zilitangaza hatua yakuondoa sheria yawatu wakaribu wa walio ambukizwa kujitenga pamoja na sheria za karantini.

"Sasa hivi, tuku katika hatua yaku kana ya janga, ambako tunataka ishi kama tulivyo fanya kabla," Profesa Baxter alieleza shirika la habari la ABC TV Jumanne.

Beijing inafanya vipimo vya watu kwa wingi baada ya mlipuko mpya wa UVIKO-19. Jumatatu, afisa wa afya aliripoti maambukizi 70 katika vitongoji 16 vya mji huo mkuu wa taifa. Nyingi ya kesi hizo 46 zilikuwa katika kitongoji cha Chaoyang.

China imechukua hatua kali zaudhibiti wa usambaaji wa UVIKO-19, Mji wake mkuu wakibiashara Shanghai imekuwa chini ya amri yamakatazo yakutoka nje kwa muda wa wiki nne zilizo pita.

Tazama video mpya kutoka China hapa.

 


 




Pata zahanati ya kupimia UVIKO-19

Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya 



Kama unahitaji msaada wa fedha, tazama chaguzi zako ni gani


Hapa kuna msaada waku saidia kuelewa maneno yakiufundi ya UVIKO-19 katika Kiswahili



Soma taarifa zote kuhusu UVIKO-19 katika Kiswahili kwenye tovuti ya SBS kuhusu Coronavirus.  

 


Share

Published

Updated

Presented by Gode Migerano

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa mpya ya UVIKO-19: Australia yaripoti vifo 42, abiria wapatwa na uviko ndani ya meli yakitalii WA | SBS Swahili