Taarifa mpya ya UVIKO-19: Mchezaji wa cricket wa Australia alazwa hospitalini baada yakuambukizwa coronavirus

Hii ni taarifa yako mpya kuhusu UVIKO-19 nchini Australia kwa 19 Aprili 2022.

Australian all-rounder Mitch Marsh (file).

Australian all-rounder Mitch Marsh (file). Source: Jason O'Brien/PA Wire.

Mchezaji wa cricket wa Australia Mitchell Marsh yuko hospitalini baada yakupatwa na COVID-19 India.

Marsh anacheza katika timu moja na muAustralia mwenza David Warner katika timu ya Delhi Capitals katika ligi kuu ya cricket ya India.

Delhi Capitals kupitia taarifa imesema wanachama wake kadhaa, wafanyakazi wakijumuishwa wamerejesha matokeo chanya ya vipimo. Wote hawana dalili za ugonjwa ila, hali zao zinafuatiliwa kwa karibu.

Biashara NSW na chama cha Biashara na Viwanda cha Victoria, vimeomba serikali husika ziondoe sharti la kujitenga kwa siku saba ambazo zipo kwa sasa, kwa watu ambao ni wakaribu wa mtu aliye ambukizwa COVID-19.

Vikundi vya biashara vime laumu masharti yakujitenga, kwa uhaba wa wafanyakazi.

Vituo vyakutoa taarifa za chanjo za UVIKO-19, vimefunguliwa ndani ya masoko makubwa na matukio katika majimbo ya New South Wales, Victoria na Queensland.

Wakaaji wanaweza pata taarifa nakuomba miadi ya chanjo zao, katika vituo vifuatavyo kuanzia 18 hadi 24 Aprili:

NSW – Penrith, Westfield Penrith

NSW – Campsie, Campsie SC

QLD – Broadbeach, Pacific Fair

QLD – Brown Plains, Grand Plaza

VIC – Dandenong, Dandenong Plaza

VIC – Narre, Warren Westfield Fountain Gate

Shirika linalo simamia maswala yakulinda umma dhidi ya hatari zakibaolojia na dharura kuhusiana na UVIKO-19 kwa Australia iliisha 17 Aprili. Inamaana kwamba wasafiri wanao ingia Australia, hawatakiwi tena kuwa na matokeo hasi ya kipimo cha UVIKO-19 kabla waje na meli za abiria zinaweza ingia Australia tena.

Kanuni za kuzuia kupandishwa kwa bei ya vipimo vya rapid antigen nazo zime isha.

Hata hivyo, wasafiri wakimataifa wanao ingia nakutoka Australia, bado wanatakiwa kutoa ushahidi wa chanjo zao mbili pamoja nakuvaa barakoa katika safari zakimataifa chini ya ushauri wamatibabu.

Wakaaji wa marekani hawatakiwi tena kuvaa barakoa ndani ya usafiri wa umma, baada ya mahakama yashirikisho kufuta sharti la miezi 14 lakuvaa barakoa jana Jumatatu.

Mji wa Shanghai umeripoti vifo vitatu vya UVIKO-19 kutoka mlipuko wa sasa ambao umetumbukiza mji huo mkubwa katika, makatazo yakutoka nje kwa muda wa wiki tatu. Hata hivyo, wasiwasi umezuliwa kuhusu usahihi wa takwimu hizo.

 

 

 

 


Soma kuhusu Chanjo za UVIKO-19 katika Kiswahili


Pata zahanati ya kupimia UVIKO-19

ACT   New South Wales   Northern Territory   Queensland   

South Australia   Tasmania   Victoria   Western Australia  

Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya 

ACT   New South Wales   Northern Territory   Queensland    

South Australia   Tasmania   Victoria    Western Australia


Jua kuhusu unachoweza na kile ambacho hauwezi fanya popote nchini Australia

Kabla uende ng'ambo, tazama masharti mapya ya usafiri na ushauri

Kama unahitaji msaada wa fedha, tazama chaguzi zako ni gani

Hapa kuna msaada waku saidia kuelewa maneno yakiufundi ya UVIKO-19 katika Kiswahili


Soma taarifa zote kuhusu UVIKO-19 katika Kiswahili kwenye tovuti ya SBS kuhusu Coronavirus.  


Share

3 min read

Published

Presented by Gode Migerano




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now