Taarifa Mpya kuhusu COVID-19: Mamlaka wataka viwango vya juu vya vipimo na chanjo

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa tarehe 17 Agosti 2021.

Jeshi la Ulinzi la Australia

Maafisa wa jeshi la Australia, wawasaidia watu walio enda kupokea chanjo katika kituo cha chanjo cha Qudos Bank Arena, NSW. Source: AAP Image/Bianca De March

  • Kesi nyingi jimboni NSW, zina wahusu watu wenye chini ya miaka 40
  • Kiongozi wa VIC atoa wito kwa viwango vya juu vya vipimo
  • Kesi mpya kumi na saba ndani ya jamii zatambuliwa ACT
  • Hakuna kesi mpya NT

New South Wales

NSW imerekodi kesi mpya 452 ndani ya jamii, kesi 50 zikiwa katika hali ambukizi zilipokuwa ndani ya jamii. Asilimia sabini ya kesi mpya ina wahusu watu wenye chini ya miaka 40. Mwanamke mwenye zaidi ya miaka 70 ambaye alikuwa haja chanjwa alifariki.

Wakaaji wa Lennox Head wame hamasishwa wapimwe wakati, wakati chembe chembe za COVID zilitambuliwa katika maji taka yaliyo fanyiwa vipimo katika kifaa cha vipimo katika eneo hilo.

Kiongozi wa NSW Gladys Berejiklian, ametoa wito maalum kwa watu wenye zaidi ya miaka 70 wakachanjwe.

Omba hapa miadi ya chanjo.

Victoria

Victoria imerekodi kesi mpya 24 ndani ya jamii, tatu kati yazo ziki ungwa na milipuko inayo julikana. Kesi kumi zilikuwa ndani ya jamii, zilipokuwa katika hali ambukizi.

Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews ameomba pawe ongezeko yavipimo hususan, katika maeneo ya vitongoji vya St Kilda, maeneo ya Port Phillip na Bayside yaki jumuishwa.

Pata hapa orodha ya sehemu zaku fanyia vipimo na orodha ya vituo vya chanjo

Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
  • Wilaya ya ACT imerekodi kesi mpya 17 ndani ya jamii, hali ambayo imefikisha idadi kamili ya kesi mjini Canberaa 45. Kwa sasa kuna karibu sehemu 100 za maambukizi ACT.
  • Northern Territory haija rekodi kesi yoyote ndani ya jamii, kutoka vipimo 1,846 vilivyo fanywa jana.
  • Queensland imerekodi kesi moja ndani ya jamii, iliyo kuwa katika karantani nyumbani.
alc covid mental health
Source: ALC

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti ya vipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

NSW Safari & usafiri and Karantini

VIC Kabali cha safariwasafiri wa ng'ambo na Karantini

ACT Usafiri na Karantini

NT Safari na Karantini

QLD Safari na Karantini

SA Safari na Karantini

TAS Safari na Karantini

WA Safari na Karantini

Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba ruhusa mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa nakuchapishwa na huduma ya mawasiliano ya Afya ya tamaduni nyingi ya NSW:

COVID-19 Vaccination Glossary
Appointment Reminder Tool.


Zahanati za chanjo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania

Northern Territory 


Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo na wilaya:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania
Northern Territory


Share

3 min read

Published

By SBS/ALC Content

Presented by Gode Migerano

Source: SBS




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now