- Tume ya ushindani na watumiaji ya Australia (ACCC) ime omba polisi ichunguze biashara kadhaa baada yakupokea zaidi ya ripoti 100, kila siku kutoka kwa wateja wanao lipishwa hela nyingi kuliko kawaida kununua vipimo vya rapid antigen.
- Mchunguzi huyo ameonya kuwa licha ya gharama ya jumla ya vipimo vya RAT kuwa kati ya $5 na $10, imeripotiwa kuwa vipimo hivyo vimekuwa viki uzwa kwa kati ya $20 hadi $30 wakati baadhi ya maduka madogo yana uza vipimo hivyo kwa zaidi ya $70.
- Waziri Mkuu Scott Morrison ata toa milioni $209 kwa malipo ya hela taslim kwa wafanyakazi wa huduma za wazee, katika jibu kwa ongezeko ya shinikizo kwa janga la UVIKO-19 linalo endelea kwa sekta hiyo ambayo ime athiriwa sana na virusi hivyo. Ila vyama vya wafanyakazi vime kosoa hatua hiyo vikisema ni jaribio lakisiasa kupata kura katika uchaguzi mkuu ujao.
- Serikali ya Victoria itafungua zahanati za chanjo katika sehemu kadhaa za kirafiki kwa watoto, kama sehemu ya mradi wakuongeza viwango vya chanjo miongoni mwa watoto kutoka mazingira magumu. Maeneo ambako zahanati hizo zitawekwa ni pamoja na katika eneo la Melbourne Zoo na Aquarium ambako samaki hufugwa.
- Tahli Gill ambaye huwakilisha Australia katika mchezo wa Curling, ata endelea na maandilizi yake ya michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi pamoja na mwenzake Dean Hewitt baada yakuponea kupata UVIKO-19. Wawili hao wame pata matokeo kadhaa hasi ya vipimo vya UVIKO-19, baada yavipimo walivyo fanya walipo wasili mjini Beijing kurejesha matokeo chanya ya UVIKO-19.
- Katika siku nne zilizo pita, maafisa walitambua kesi za UVIKO-19 miongoni mwa wachezaji na watu wanao husika katika michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya 2022 mjini Beijing, ambayo ina anza kesho.
- Baraza la mawaziri la New Zealand linakutana leo kukamilisha tarehe zakufungua tena mipaka ya nchi hiyo. Kwa sasa raia wanao rejea nchini humo, lazima wawe ndani ya hoteli za karantini kwa muda wasiku 10 wanako jitenga, na kwa sasa kuna uhaba wa nafasi katika hoteli hizo, hali ambayo imesababisha mstari mrefu wa watu wanao subiri kurundi nchini humo.
Takwimu za UVIKO-19:
Jimboni NSW kwa sasa kuna idadi ya watu 2,749 wanao hudumiwa hospitalini wakiwa na virusi na wagonjwa 183 wanahudumiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti, wagonjwa 70 wanatumia mashine kwa ajili yakupumua. Kumekuwa vifo vipya 30 na idadi ya maambukizi mapya ya virusi jimboni humo ni 12,818.
Jimboni Victoria, watu 851 wako hospitalini na wagonjwa 106 wamo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti. Kumeripotiwa vifo 34 pamoja na idadi ya maambukizi mapya 11,311.
Jimboni Queensland, kuna idadi ya watu 868 hospitalini, na wagonjwa 50 wamo ndani ya kitengo cha huduma ya wagonjwa mahtuti na kumeripotiwa kesi mpya 7,588 za maambukizi- ya virusi.
Jimboni Kusini Australia watu 273 wamo hospitalini, na watu 22 wanapokea huduma katika kitengo cha wagonjwa mahtuti. Vifo 3 vimeripotiwa pamoja na idadi ya maambukizi mapya 1266.
Jimbo la Tasmania limerikodi kesi mpya 699, watu 16 wamo hospitalini, na mtu mmoja anapokea huduma katika kitengo cha wagonjwa mahtuti, na hapaja ripotiwa vifo vyovyote jimboni humo.
Majimbo kadhaa yame andaa fomu zaku sajili vipimo vya RAT.
Karantini na vizuizi jimbo kwa jimbo
Safari
Msaada wakifedha
Kuna mageuzi kwa malipo ya janga ya UVIKO-19, punde jimbo linapo fikisha asilimia 70 na 80 ya watu ambao wamepata chanjo kamili: Kupata msaada wakati wa UVIKO-19 kutoka shirika la Services Australia katika lugha yako
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60 sbs.com.au/coronavirus
- Pata hapa miongozo inayostahili kwa jimbo au wilaya yako: NSW, Victoria, Queensland, Western Australia, South Australia, Northern Territory, ACT, Tasmania.
- Pata hapa taarifa kuhusu chanjo ya UVIKO-19 katika lugha yako.