Taarifa mpya ya COVID-19: Jimboni NSW ‘maisha yatakuwa bora’ punde itakapo timiza 80% ya chanjo, Victoria yaongeza muda wa utoaji wa mifuko ya misaada

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 5 Septemba 2021.

Jamii zakwanza zapewa chanjo ya COVID-19 mjini Sydney

Wanachama wa jamii zawatu wa asili, wapokea chanjo za Covid-19 katika zahanati iliyo jenga katika kituo chakitaifa cha ubora wa asili. Source: AAP/Dan Himbrechts

  • NSW yafikia utoaji wa 40% ya dozi mbili za chanjo
  • Victoria yatangaza msaada kwa jamii ambazo katika hali mbaya
  • ACT yaripoti kesi mpya 15 ndani ya jamii
  • Queensland yaripoti kesi moja mpya ndai ya jamii

New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 1485 ndani ya jamii, na vifo vitatu. Kuna zaidi ya watu elfu moja ndani ya hosptiali, 175 wako ndani ya kitengo cha hali mahtuti, na 72 kati yao wanapokea msaada wa kupumua kwa mashine.

NSW kwa sasa imefikia 40% ya watu ambao wamepokea dozi mbili na 73% ya watu ambao wamepokea dozi ya kwanza ya chanjo. Kiongozi wa jimbo hilo Gladys Berejiklian amesema, "bila shaka jimbo hilo halitakuwa na makatazo ya jimbo zima tena", wakati 80% ya chanjo itakuwa imetolewa ila, ameonya kuwa idadi ya kesi itaongezeka katika wiki mbili zijazo.

Bonyeza hapa kupata miadi ya chanjo yako leo. 

Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 183 ndani ya jamii, kesi 101 zikiungwa na milipuko inayo julikana.

Waziri Luke Donnellan alitangaza ongezeko uwekezaji wa $27 milioni kwa kuendeleza mfuko wa msaada kwa jamii ambazo ziko katika hali mbaya.

Pata hapa kituo cha chanjo karibu yako.

Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita 

  • ACT yarekodi kesi mpya 15, 13 kati yazo zikiungwa na mlipuko unao julikana. Kesi sita zilikuwa ndani ya karantini muda wote zilikuwa katika hali ambukizi.
  • Kesi moja mpya imerekodiwa Queensland, ikimhusu mama ya mtoto aliye patwa na virusi jana.
  • Serikali ya WA yataka angalau 80% ya wakaaji wa Magharibi Australia wanao stahiki wachanjwe kabla, serikali hiyo iweke tarehe yaku ondoa vizuizi vigumu vya mpaka.
How can I shop safely
Source: ALC

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

ACT Usafiri na Karantini
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 
ACT 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 
ACT 
 

Share

Published

By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service