Taarifa mpya kuhusu UVIKO-19: Wilaya ya Kaskazini uangeza muda wa makatazo kesi mpya ziki endelea kuibuka

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 23 Novemba 2021.

Kiongozi wa Wilaya ya Kaskazini Michael Gunner azungumza na waandishi wa habari katika bunge la NT mjini Darwin

Kiongozi wa Wilaya ya Kaskazini Michael Gunner, azungumza na waandishi wa habari katika bunge la NT mjini Darwin. Source: AAP Image/Aaron Bunch

  • Wilaya ya Kaskazini kuendelea chini ya vizuizi au sheria zakuto toka hadi 4 Disemba, baada ya wilaya hiyo kurekodi kesi mpya 3 za maambukizi ndani ya jamii, ambayo moja yazo ilimhusu mtoto mchanga.
  • Kiongozi wa Queensland Annastacia Palaszczuk amesema safari za haraka za kwenda Sydney ni marufuku, hadi wakati jimbo la Queensland litakapo fikisha lengo la 90% ya chanjo.
  • NSW imeomba mageuzi kwa mfumo wa vipimo kwa wasafiri wa ndani ya nchi.
  • Jimbo la Kusini Australia limefungua usafiri bila sharti la karantini, kwa wasafiri kutoka NSW, ACT na Victoria. Idadi ya wasafiri 43,000 wameomba ruhusa yakusafiri kupitia tovuti ya EntryCheck tangu mchana wa Ijumaa. 
  • Watu wanao safiri kutoka halmashauri za jiji zenye chini ya kiwango cha 80% ya chanjo, na ambako bado kuna maambukizi ya virusi ndani ya jamii, itabidi waingie katika karintini jimboni Kusini Australia.

TAKWIMU ZA UVIKO-19:

Victoria imerekodi kesi mpya 827 za maambukizi ndani ya jamii pamoja na vifo 19. Kati ya vifo hivyo 17 walikuwa hawaja chanjwa.
NSW imerekodi kesi mpya 173 za maambukizi ndani ya jamii, pamoja na vifo viwili. 
ACT imerekodi kesi mpya 19 ndani ya jamii.


Karantini na vizuizi katika kila jimbo na wilaya:

Usafiri

Taarifa kwa wasafiri wakimataifa na taarifa za usafiri wa UVIKO-19 katika lugha yako

Msaada wakifedha

Kuna mageuzi kwa malipo ya janga ya UVIKO-19, punde majimbo yatakapo fikisha viwango vya 70% na 80% ya watu ambao wame pata chanjo kamili: Kupata msaada wakati wa UVIKO-19 kutoka Services Australia katika lugha yako


 


 





Tazama rasilimali zilizo tafsiriwa nakuchapishwa na Huduma ya mawasiliano ya idara ya afya ya tamaduni nyingi ya NSW:



Pata hapa taarifa kuhusu zahanati za chanjo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 
ACT 

Share

Published

Updated

By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service