Taarifa mpya ya UVIKO-19: Chanjo ya Novavax yawasili Australia

Hii ni taarifa yako mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 8 Februari.

Mwanamke apokea chanjo ya UVIKO-19 katika zahanati ya Sydney Road Family Medical Practice mjini Balgowlah 10 Januari 10, 2022 in Sydney, Australia.

Mwanamke apokea chanjo ya UVIKO-19 katika zahanati ya Sydney Road Family Medical Practice mjini Balgowlah 10 Januari 10, 2022 in Sydney, Australia. Source: Getty Images AsiaPac

  • Mzigo wa kwanza wenye chanjo ya Novavax umewasili Australia kutoka Singapore. Mzigo huo una dozi za kwanza milioni tatu ambazo zita tolewa kote nchini 21 Februari.
  • Idadi ya maafisa 1,700 wa jeshi la ulinzi la Australia, wata tumwa kupunguza shinikizo kwa mfumo wa huduma ya wazee hata hivyo, watetezi wanasema haitoshi tu kupunguza uhaba wa wafanyakazi.
  • Jimboni NSW, 44% ya umma unao fuzu kwa sasa wame pata dozi yao ya tatu ya chanjo ya UVIKO. Jimboni Victoria 46% ya watu wazima wame pokea dozi zao za tatu.
  • Serikali ya Victoria ita tanua upatikanaji wa vifaa vya vipimo vya rapid antigen, kama familia za watoto wenye miaka mitatu hadi tano wanao pokea huduma ya watoto, wata peleka vipimo hivyo nyumbani katika wiki zijazo.
  • Wakati idadi ya kesi za maambukizi zinaendelea kupungua katika majimbo mengi, Wilaya ya Kaskazini ina kiwango cha juu nchini Australia cha watu walio lazwa hospitalini kwa sababu ya hali zinazo husiana na UVIKO.

Takwimu za UVIKO-19:

NSW imeripoti idadi ya wagonjwa 2068 wamelazwa hospitalini, wagonjwa 132 kati yao wakiwa ndani ya kitengo cha hali mahtuti. Kuna vifo vipya 18 na, kesi mpya 9,690 za maambukizi ya UVIKO-19.

Jimboni Victoria, watu 575 wame lazwa hospitalini, watu 72 wako ndani ya kitengo cha hali mahtuti. Kume ripotiwa vifo 20 pamoja na maambukizi mapya 9,785.

Jimboni Queensland watu 705 wame lazwa hospitalini, idadi hiyo inajumuisha watu 45 ambao wamo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti, vifo 12 vimeripotiwa pamoja na kesi mpya 5,178 za maambukizi.

Nalo jimbo la Tasmania lina watu 15 ambao wame lazwa hospitalini, kuna kesi mpya 601 za maambukizi na jimbo hilo halija ripoti vifo vyovyote.

Kwa hatua zilizopo kwa sasa katika jibu la janga la UVIKO-19 katika lugha yako, bonyeza hapa.


Majimbo kadhaa yana fomu zaku sajili matokeo ya vipimo vya RAT.

Karantini na vizuizi jimbo kwa jimbo

Safari

Msaada wakifedha

Kuna mageuzi kwa malipo ya janga ya UVIKO-19, punde majimbo yanapo fikia viwango vya 70% na 80%  ya watu ambao wame pata chanjo kamili: Kupata msaada wakati wa UVIKO-19 kutoka Services Australia katika lugha yako


 


 



Tazama rasilimali zilizo tafsiriwa nakuchapishwa na shirika la NSW Multicultural Health Communication Service


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya

NSW 
ACT 

Share

Published

Presented by Gode Migerano

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa mpya ya UVIKO-19: Chanjo ya Novavax yawasili Australia | SBS Swahili