Taarifa mpya kuhusu COVID-19: NSW yavunja rekodi tena ya kila siku ya kesi, na kesi zaendelea kuongoezeka katika maeneo ya kanda ya Victoria

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa tarehe 22 Agosti 2021.

Watu wafanya mazoezi mjini Sydney, Jumapili, 22 Agosti, 2021

Watu wafanya ma.zoezi mjini Sydney, Jumapili, 22 Agosti, 2021. Source: AAP Image/Bianca De Marchi

  • NSW yarekodi kesi mpya 830 za COVID-19 na vifo vitatu 
  • Kesi mpya 65 za COVID-19 zarekodiwa Victoria, kesi 21 zime unga na mlipuko wa Shepparton    
  • ACT yarekodi kesi mpya 19 za coronavirus
  • Queensland haija rekodi kesi yoyote ya COVID-19 katika masaa 24 yaliyo pita

New South Wales

NSW yaweka rekodi nyingine yakila siku ya kesi mpya 830 za COVID-19.  

NSW ilirekodi pia vifo vitatu ambavyo viliwahusu wanaume wawili, mmoja akiwa na miaka 60 na mwingine 70 wawili hao wakiwa walikuwa wamepokea dozi ya kwanza ya chanjo ya COVID-19, pamoja na mwanamke mwenye miaka 80 ambaye alikuwa haja chanjwa na alikuwa mtu wakaribu wa aliyekuwa na virusi hivyo. Kupitia vifo hivyo vitatu, idadi kamili ya vifo kupitia mlipuko wa sasa imefika 71.

Kwa sasa kuna watu 550 hospitalini ambao wanapokea matibabu ya COVID-19, watu 94 kati yao wakiwa katika hali mahtuti.

Waziri wa Afya Brad Hazzard amesema NSW imerekodi viwango "visivyo vya kawaida" vya chanjo katika siku chache zilizo pita.

Omba miada yako ya chanjo leo. 

Victoria

Victoria imerekodi kesi mpya 65 za COVID-19, kesi 55 ziki ungwa na milipuko ya sasa na kesi 10 zina fanyiwa uchunguzi. 

Ni kesi 12 tu ambazo zilikuwa zinajitenga kwa muda wato ambao zilikuwa katika hali ambukizi.

Katika kesi zilizo sajiliwa leo, angalau 21 zili ungwa na mlipuko katika mji wa kanda wa Shepparton.  

Wakaaji wa Victoria waliamka leo asubuhi nakupata, jimbo zima likiwa chini ya vizuizi. 

Jeshi la Polisi la Victoria limeripoti zaidi ya watu 200 wamekamatwa na maafisa sita wa polisi walijeruhiwa katika maandamano dhidi ya kufungiwa ndani mjini Melbourne jana.

Pata hapa orodha ya sehemu za maambukzi na orodha ya vituo vya chanjo

Hali ilivyokuwa katika masaa 24 nchini Australia

  • ACT imerekodi kesi mpya 19 za COVID-19, kesi sita zilikuwa ndani ya jamii wakati zilikuwa katika hali ambukizi. Mwanafunzi wa chuo cha ANU alipatwa na virusi hivyo ila alikuwa akijitenga.
  • Queensland imekuwa na siku nyingine ambayo haija rekodi kesi yoyote, wakati kuna kesi 39 zinazo tibiwa. 
Self-Isolation can impact our mental health and wellbeing.
Source: ALC

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti ya vipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

NSW Safari & usafiri na Karantini

VIC Kibali cha safariWasafiri wa ng'ambo na Karantini

ACT Usafiri na Karantini

NT Safari na Karantini

QLD Safari na Karantini

SA Safari na Karantini

TAS Safari na Karantini

WA Safari na Karantini

Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa ya ziada kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa, ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali na huchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Pata hapa rasilimali zilizo tafsiriwa nakuchapishwa na huduma yamawasiliano ya afya ya tamaduni nyingi ya NSW:

COVID-19 Vaccination Glossary
Appointment Reminder Tool.


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania

Northern Territory 


Taarifa kuhusu malipo ya janga katika lika jimbo na wilaya:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania
Northern Territory 


Share

3 min read

Published

By SBS/ALC Content

Presented by Gode Migerano

Source: SBS




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now