Taarifa mpya kuhusu COVID-19: NSW yapanga kufungua mipaka yakimataifa kufikia Krismasi, Victoria yathibitisha kuanzishwa kwa vituo vya chanjo

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa tarehe 12 Septemba 2021.

Sydney International Airport during Covid-19

Msafiri ajandaa kuabiri basi la karantini, katika uwanja wa ndege wakimataifa wa Sydney, Jumatano, Septemba 8, 202 Source: AAP Image/Joel Carrett

  • Kuanzia kesho baadhi ya vizuizi vitaregezwa jimboni NSW
  • Jimboni Victoria, kuna miadi 7,000 ya dozi ya kwanza ya chanjo ya Pfizer
  • ACT imerekodi kesi mpya 15 na Queensland haijawa na kesi yoyote mpya ndani ya jamii 

New South Wales

NSW imerekodi kesi mpya 1,262 ndani ya jamii, pamoja na vifo saba.

Kuanzia tarehe 13 Septemba, idadi ya wakaaji 5 ambao wame pokea chanjo kamili wanao ishi nje ya halmashauri 12 za wasiwasi wataruhusiwa kukutana nje ya nyumba zao. Wanao ishi ndani ya halmashauri hizo za wasiwasi wanaweza enda nje kufanya mazoezi au katika bustani, pamoja na wanachama wa nyumba zao ambao wame pokea chanjo kamili, kwa muda wa masaa mawili kila siku kwa nyongeza ya muda wa mazoezi bila kikomo.

Kiongozi wa jimbo hilo Berejiklian amesema, jimbo hilo lina lengo lakufungua mipaka yakimataifa kufikia wakati wa krisamasi, wakati inatarajiwa 78% ya umma wenye zaidi ya miaka 16 watakuwa wame pokea dozi ya kwanza ya chanjo, na 45.58% ya umma itakuwa imepokea chanjo kamili.

Bonyeza hapa kuomba miadi yako ya chanjo leo. 

Victoria

Victoria imerekodi kesi mpya 392 mpya ndani ya jamii.

Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amesema kuna miadi 7,000 ya dozi za kwanza za Pfizer, katika wiki zijazo ndani ya zahanati zinazo simamiwa na serikali ya jimbo hilo.

Vituo vipya vya chanjo vitafunguliwa kote jimboni Victoria ndani ya shule nane na katika halmashauri za jiji za; Hume, Dandenong na Casey, kanisa la Greek Orthodox Church katika kitongoji cha Thornbury, hekalu laki Hindu katika kitongoji cha Mill Park pamoja na katika msikiti ambao uko katika kitongoji cha Newport.

Pata hapa kituo cha chanjo kilicho karibu yako.                                                                                                      

Hali ilivyo kuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
  • Waziri Mkuu Scott Morrison ametangaza uwepo wa dozi milioni za ziada za, chanjo ya COVID-19 za Moderna, ambazo zime pendekezwa kwa kila mtu mwenye zaidi ya miaka 12.
alc covid mental health
Source: ALC

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

NSW Safari & usafiri na Karantini

VIC Vibali vya safariWasafiri wa ng'ambo na Karantini

ACT Usafiri na Karantini

NT Safari na Karantini

QLD Safari na Karantini

SA Safari na Karantini

TAS Safari na Karantini

WA Safari na Karantini

Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:

COVID-19 Vaccination Glossary
Appointment Reminder Tool.


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania

Northern Territory 


Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania
Northern Territory


Share

3 min read

Published

Updated

By SBS/ALC Content

Presented by Gode Migerano

Source: SBS




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now