Taarifa mpya kuhusu COVID-19: NSW yatangaza "ruhusa ya marafiki", Victoria yapitisha idadi ya kesi 600 za kila siku

Hii ni taarifa yako mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 21 Septemba 2021.

Extremists' blasted as hundreds march in Melbourne during another vaccine protest

Extremists' blasted as hundreds march in Melbourne during another vaccine protest Source: AAP/James Ross

 Miji ya Byron, Kempsey na Tweed jimboni NSW yarejea tena katika amri yakuto toka nje

  • Victoria kwa sasa ina kesi 6,000 za COVID-19
  • ACT yatangaza uwekezaji wa ziada kwa huduma za afya ya akili
 


New South Wales 

NSW imerekodi kesi mpya 1,022 ndani ya jamii pamoja na vifo 10. Kwa sasa, 53% ya wakaaji wanao stahiki jimboni humo wame pata chanjo kamili.

Miji ya Byron Shire, Kempsey na halmashauri ya jiji ya Tweed zita ingia katika amri yakuto toka ndani kwa muda wa siku saba kuanzia saa kumi na moja jioni ya leo, baada ya kesi chanya ya COVID kutoka Sydney kutembelea jamii kadhaa za pwani ya kaskazini ya NSW.

Kuanzia leo, kundi la watu watatu wenye chini ya miaka 18 wana weza tembeleana nyumbani mwao kama, wanaishi katika eneo la mzunguko wa kilomita tano au katika kitongoji kimoja. Ruhusa hiyo yamarafiki kutembeleana, imetolewa tu kwa nyumba ambako watu wazima wote wame pokea chanjo kamili.

Shirika la Msalaba Mwekundi la Australia linatoa msaada wakifedha wa mara moja kwa watu ambao wana viza za muda mfupi au watu ambao hawana viza na wame athiriwa kwa amri zakuto toka nje jimboni NSW.

Bonyeza hapa kuomba miadi yako ya chanjo leo. 

Victoria

Victoria imerekodi kesi mpya 603 ndani ya jamii pamoja na kifo kimoja.

Katika maeneo ya jiji la Melbourne, Geelong, Surf Coast, Ballarat na Mitchell Shire, sekta ya ujenzi imefungwa kwa muda wa wiki mbili baada ya milipuko kadhaa ya maambukizi iliyo ungwa na sekta hiyo ya ujenzi. 

Kwa sasa kuna idadi ya kesi chanya 403 za maambukizi, ambazo zina ungwa na sekta hiyo, na pia zina husiana na maeneo 186 ya ujenzi.

Victoria inatarajia kupokea zaidi ya chanjo laki tatu za Moderna zitakazo sambazwa kote jimboni humo.

Pata hapa kituo cha chanjo kilicho karibu yako.   

Australian Capital Territory

Wilaya ya ACT imerekodi kesi mpya 16 ndani ya jamii.  

Kiongozi wa ACT Andrew Barr ametangaza uwekezaji wa ziada wa dola milioni 14, kwa mashirika yanayo toa huduma za msaada wa afya ya akili, pombe pamoja na mihadarati ndani ya wilaya hiyo.

 

 

Domestic violence during COVID-19 pandemic
Domestic infographic Source: SBS

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

ACT Usafiri na Karantini
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 
ACT 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 
ACT 

Share

Published

Updated

By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa mpya kuhusu COVID-19: NSW yatangaza "ruhusa ya marafiki", Victoria yapitisha idadi ya kesi 600 za kila siku | SBS Swahili