Taarifa mpya ya UVIKO-19: Waziri wa Afya wa NSW asema ni 'ukichaa' kutochukua dozi ya jeki; majimbo yatathmini tena sheria zakuvaa barakoa

Hii ni taarifa yako mpya ya UVIKO-19 nchini Australia kwa 5 Julai.

NSW Premier Dominic Perrottet and Minister for Health Brad Hazzard during a visit to Homebush vaccination hub, in Sydney, Sunday, February 6, 2022 (AAP Image/Pool, Gaye Gerard ) NO ARCHIVING

NSW Health Minister Brad Hazzard (left) said it's "crazy" to skip a booster dose as the new "pesky little variants" can reinfect people. (file) Source: AAP Image/Pool, Gaye Gerard )

Jumanne, Australia iliripoti vifo 46 vya UVIKO-19, vilivyo jumuisha vifo 16 Victoria, 14 New South Wales (NSW) na 11 Queensland.

Idadi ya watu wenye UVIKO-19 walio lazwa hospitalini, inaendelea ongezeka katika majimbo na wilaya zote nchini Australia.

Tasmania ilishuhudia ongezeko kubwa kwa idadi ya maambukizi mapya. Iliripoti kesi mpya 1,588 za UVIKO-19 Jumanne, kulingana na kesi 1,094 Jumatatu.  

Queensland iliripoti watu 710 wenye UVIKO-19 walio lazwa hospitalini Jumanne, kulingana na watu 598 Jumatatu. Hiyo ni idadi kubwa zaidi ya walio lazwa hospitalini katika miezi nne iliyopita.

Tazama maendeleo mapya ya kesi mpya za UVIKO-19, watu wanao lazwa hospitalini pamoja na vifo nchini Australia hapa.


Waziri wa Afya wa NSW Brad Hazzard amesema ni "ukichaa" kukosa kuchukua chanjo ya UVIKO-19, wakati aina mpya tata zavirusi (BA.4 na BA.5) vinaweza waambukiza watu ambao wame ugua tayari coronavirus. 

Amekiri kuwa chanjo hazi zuii uambukizaji ila, chanjo za jeki zinaweza linda dhidi ya magonjwa mabaya. 

“Kama umepata dozi mbili, au moja, na hauchukui ya tatu, kusema kweli wewe ni kichaa," waziri huyo alisema.

Bw Hazzard aliwashauri wakaaji wachukue hatua za msingi kama kunawa mikono mara kwa mara, kuvaa barakoa katika sehemu za umma na, kubaki nyumbani kama unaumwa.

Aliongezea kuwa 56% (1,232) ya vifo vinavyo husiana na UVIKO mwaka huu, viliwahusu watu ambao wamechukua chanjo mbili au chache. Aliongezea kuwa jimbo hilo lilikuwa katika mwanzo wa wimbi la tatu la Omicron, ambalo lina uwezekano wakufikia kilele mwisho wa Julai au manzo wa Agosti.

Kamati kuu ya ushauri wa chanjo ya Australia, inakutana leo, kati ya ongezeko la wito kwa dozi ya chanjo ya nne kwa wafanyakazi wa huduma ya afya na wengine.

Kiongozi wa jimbo la Victoria, Dan Andrews amesema haitakuwa rahisi zaidi kwa ATAGI, kupendekeza dozi ya chanjo ya nne wakati Wa Australia wanaweza kuwa na chanjo maalum ya Omicron katika miezi ijayo. 

Bw Andrews ameongezea kuwa shinikizo la sasa kwa mfumo wa afya ni mubaya. Alitoa kesi imara kwa dozi ya chanjo ya nne kwa wafanyakazi wa huduma ya afya.

Baadhi yamajimbo na wilaya zinazingatia wazo lakurejesha amri zakuvaa barakoa, wakati kuna ongezeko la idadi ya maambukizi mapya, kulazwa hospitalini pamoja na vifo.

Majimbo ya Kusini Australia na NSW, yameiomba serikali ya shirikisho iregeze sheria za ustahiki kwa dawa za UVIKO-19. 

Kwa sasa, tiba hiyo inatolewa tu kwa wazee, watu kutoka jamii zawa Aboriginal na Torres Strait Islands wenye mika 50 au zaidi, na mambo mengine mawili ya hatari pamoja na watu wenye miaka 18 au zaidi ambao kinga zao za mwili zime athirika kwa wastan au sana.

 

 


 




Pata zahanati ya vipimo vya UVIKO-19

Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya 



Kama unahitaji msaada wa fedha, tazama chaguzi zako ni gani


Hapa kuna msaada waku saidia kuelewa maneno yakiufundi ya UVIKO-19 katika Kiswahili



Soma taarifa zote kuhusu UVIKO-19 katika Kiswahili kwenye tovuti ya SBS kuhusu Coronavirus.  


Share

Published

Presented by Gode Migerano

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service