Taarifa mpya kuhusu COVID-19: NSW yapita 80% ya lengo ya chanjo wakati Victoria yatangaza kampeni ya $21milioni

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 19 Oktoba 2021.

Picha za wafanyakazi wa mstari wa mbele zamulikwa kwenye paa za Sydney Opera House na umma wa NSW ulio chanjwa kuadhimisha kufikisha lengo la 80% ya chanjo.

Picha za wafanyakazi wa mstari wa mbele zamulikwa kwenye paa za Sydney Opera House na umma wa NSW ulio chanjwa kuadhimisha kufikisha lengo la 80% ya chanjo. Source: AAP/DEAN LEWINS

  • Victoria yatangaza mfuko wa $21milioni kupiga jeki viwango vya chanjo
  • Ongezeko ya kesi katika kanda ya NSW yazua wasiwasi
  • ACT yatangaza uamuzi wakuregeza vizuizi

Victoria

Victoria imerekodi kesi mpya 1,749 za maambukizi ya COVID-19 na vifo 11.

89.4% ya umma wenye zaidi ya miaka 16 jimboni humo wamepokea dozi ya kwanza ya chanjo, na 67.2% wamepokea dozi zote mbili.

Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews ametangaza mfuko wa uwekezaji wa $21 milioni kupiga jeki chanjo, kujumuisha zahanati za ziada za chanjo, kuomba miadi ya, usafiri na mbinu mbadala zinapo hitajika katika jamii.

Serikali ya Victoria imethibitisha itaongeza muda mfupi wakujitenga, kwa orodha yake ya mageuzi ya sheria, jimbo hilo litakapo fikisha kiwango cha 70% ya lengo ya watu ambao wamepata chanjo mbili.

Bonyeza hapa kuomba miadi ya chanjo yako leo. 

New South Wales

New South Wales imerekodi kesi mpya 273 za maambukizi ndani ya jamii pamoja na vifo vinne.

Chini ya 75% ya watoto wenye miaka kati ya 12-15 wamepokea dozi yao ya kwanza ya chanjo ya COVID-19, wakati 35.5% yao wamepokea chanjo kamili.

Jimbo hilo limepitisha pia lengo la 80% ya chanjo kamili kwa umma wenye zaidi ya miaka 16.

Afisa Mkuu wa Afya Dr Kerry Chant amesema ongezeko ya kesi za maambukizi katika maeneo ya kanda, inaendelea kuwa sehemu ya wasiwasi na jamii imehamasishwa ichanjwe.

Pata kituo cha chanjo karibu yako.

ACT

ACT imerekodi kesi mpya 24, kesi 21 kati yazo zina ungwa na mlipuko wa sasa.

Wilaya hiyo imetangaza uamuzi wakuregeza vizuizi vya COVID-19, kama jibu kwa 80% ya chanjo kamili ya umma wenye miaka 12 na zaidi.

Biashara zote za rejareja, na biashara mhimu pamoja na zisizo mhimu, zitaruhusiwa kufunguliwa kuanzia saa 5:59 usiku wa Alhamisi 21 Oktoba.

Bonyeza hapa kuomba miadi ya chanjo yako leo. 

Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita

  • Queensland imeweka wazi mipango kwa usafiri wa ndani nakimataifa, jimbo hilo litakapo fikisha kiwango cha 70%, 80% na kisha 90% ya umma unao stahiki ambao umepata chanjo kamili.

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

NSW Safari & usafiri na Karantini

VIC Vibali vya safariWasafiri wa ng'ambo na Karantini

ACT Usafiri na Karantini

NT Safari na Karantini

QLD Safari na Karantini

SA Safari na Karantini

TAS Safari na Karantini

WA Safari na Karantini

Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:

COVID-19 Vaccination Glossary
Appointment Reminder Tool.


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania

Northern Territory 


Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania
Northern Territory


Share

3 min read

Published

By SBS/ALC Content

Presented by Gode Migerano

Source: SBS




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now