Taarifa mpya kuhusu COVID-19: NSW yasihi jamii zawa Aboriginal zichanjwe, Victoria yaharakisha kutoa chanjo kwa wanafunzi wa kidato cha 12

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa tarehe 7 Septemba 2021.

Australian Wiradjuri elder been vaccinated

Source: AAP Image/Dan Himbrechts

  • Red Cross yatoa msaada wa fedha kwa wakaaji wa eneo la Greater Sydney wenye viza za muda mfupi
  • Victoria yaweka mfumo wa kipaumbele cha utoaji wa chanjo kwa wanafunzi wa kidato cha 12
  • Miadi ya ziada kwa chanjo na vipimo yatolewa kwa wakaaji wa Canberra wenye ulemavu
  • Majimbo ya Kusini Australia na Queensland hayajawa na kesi yoyote mpya

New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 1,220 za maambukizi ndani ya jamii, pamoja na vifo vinane.

Aunty Pauline Deweerd ni Mkurugenzi wa kitengo cha Afya yawa Aboriginal, katika hospitali ya St Vincent. Ame hamasisha jamii zawa Aboriginal zichanjwe haraka iwezekanavyo wakati mamlaka wanatarajia siku saba za wastan za takriban kesi mpya 1,500 katika mwezi wa Septemba.

Shirika la Australian Red Cross limetoa msaada wa malipo ya mara moja ya $400 kwa watu wenye viza za muda mfupi, au watu ambao hawana viza na wame athiriwa na makatazo ya Greater Sydney, kupitia mradi wa msaada wa magumu.

Bonyeza hapa kuomba miadi yako ya chanjo leo.

Victoria
Victoria imerekodi siku nyingine ya kesi 246 za maambukizi mapya ndani ya jamii, hali ambayo imefikisha idadi ya kesi zinazo shughulikiwa jimboni humo 1,786.

Kuanzia leo kama sehemu ya siku kumi ya mfumo wa kipaumbele cha upatikanaji wa chanjo, mamlaka wanalenga kuwachanja wanafunzi wote wa kidato cha 12, na angalau dozi moja kabla ya mitihani yao ya mwisho. Miadi ya chanjo ya Pfizer ilifunguliwa kwa wanafunzi wa kidato cha 12, walimu, wasimamizi pamoja na watathmini wa mitihani Jumatatu, 6 September.

Pata hapa, kituo cha chanjo kilicho karibu yako.

Australian Capital Territory
Wilaya ya ACT imerekodi kesi mpya 19 ndani ya jamii, kesi sita kati yazo zilikuwa ndani ya jamii zilipokuwa katika hali ambukizi.

Serikali ya The ACT inatoa upatikanaji bora wa miadi kwa chanjo na vipimo, kwa watu wenye ulemavu kwaku hamisha zahanati ya upataji na hisia katika kituo cha afya cha Weston Creek Community Health Centre.


Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

ACT Usafiri na Karantini
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 
ACT 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 
ACT 
 

Share

Published

By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service