Taarifa mpya kuhusu COVID-19: NSW ya ahidi uhuru zaidi kwa wakaaji walio chanjwa, Vic yapanua upatikanaji wa chanjo

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 24 Agosti 2021.

drive-through testing site at Shepparton Sports Precinct in Shepparton, Victoria, Tuesday, August 24, 2021.

صف رانندگان در پشت یک کلینیک سواره آزمایش کرونا در شهر شیپرتون Source: AAP Image/Daniel Pockett

  • NSW imetoa dozi milioni sita za chanjo 
  • Victoria yapanua upatikanaji wa chanjo
  • ACT yarekodi idadi yake kubwa zaidi ya kesi
  • Queensland yarekodi kesi mpya mbili ndani ya jamii

New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 753 ndani ya jamii, angalau kesi 49 zilikuwa ndani ya jamii katika hali ambukizi. 

Kiongozi wa NSW Gladys Berejiklian amesema jimbo lake limekamilisha utoaji wa chanjo milioni sita, yenye maana kwamba asilimia 60 ya umma imepokea dozi ya kwanza ya chanjo.

Katika maeneo 12 ya halmashauri za jiji zenye wasiwasi, watu wenye kati ya miaka 16 na 39, na wafanyakazi katika sekta ya ulemavu na huduma yamalezi yawatoto, wanapewa kipaumbele kufanya miadi ya chanjo.   

Mamlaka wa Afya watatangaza uhuru zaidi baadae wiki hii, kwa wakaaji ambao wame pokea chanjo kamili. Fanya miadi yako ya chanjo leo.

Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 50 ndani ya jamii, kesi kumi zikuwa hazi ungwi na milipuko inayo julikana. Kesi thelathini na tisa zilikuwa ndani ya jamii wakati zilikuwa katika hali ambukizi.

Kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amesema mtu yeyote mwenye miaka 16 na zaidi wata stahiki kupokea chanjo za Pfizer au AstraZeneca katika vituo vya chanjo vinavyo simamiwa na serikali ya jimbo kuanzia Jumatano, 25 Agosti 2021.  

Australian Capital Territory
Wilaya ya ACT imerekodi kesi mpya 30 ndani ya jamii, kesi 17 zikiwa zilikuwa ndani ya jamii katika hali ambukizi.

Maeneo ya vipimo kama Kambah na Brindabella Business Park, zitafunguliwa tena kesho baada yakufungwa kwa sababu ya hali mbaya ya hewa.

Bonyeza hapa kupata orodha ya sehemu za maambukizi. Unaweza tazama ustahiki wako wa chanjo ya COVID-19 hapa.

Hali ilivyo kuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
  • Queensland yarekodi kesi mbili mpya, ambazo bado zinafanyiwa uchunguzi. 
  • Taasisi ya The Doherty Institute, imesisitiza kuwa itakuwa salama kwa Australia kufunguliwa tena, kwa viwango vya kati asilimia 70-80 ya chanjo, bila kujali idadi ya kesi, ilimradi hatua za afya ya umma zina endelea kusalia.

Karantini, safari, zahanati zavipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti ya vipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

ACT Usafiri na Karantini
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba ruhusua mtandaoni Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua zampito kwa safari zakimataifa ambazo hufanyiwa tathmini mara kwa mara na serikali nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilimali zilizo tafsiriwa nakuchapishwa na huduma ya mawasiliano ya afya tamaduni nyingi ya NSW:


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 
ACT 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo na wilaya yako:

NSW 
ACT 

Share

Published

By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service