Taarifa mpya kuhusu COVID-19: Mamlaka jimboni NSW na Queensland wahamasisha watu wabaki nyumbani

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia ya 3 August 2021.

Zahanati ya chanjo ya AstraZeneca katika kitongoji cha Wattle Grove

Zahanati ya chanjo ya AstraZeneca bila miadi katika kitongoji cha Wattle Grove, NSW Source: AAP Image/Joel Carrett

  • NSW yalenga kutoa dozi milioni 6 za chanjo kufikia mwisho wa Agosti.
  • Idadi ya wanao ugua jimboni Queensland yaongezeka hadi watu 47.
  • Victoria yarekodi kesi nne mpya.
  • Serikali ya shirikisho yatoa msaada wa ziada wa malipo ya COVID.

New South Wales

NSW imerekodi kesi mpya 199 ndani ya jamii, na angalau kesi 50 ndani ya jamii zilikuwa katika hali ambukizi.

Afisa Mkuu wa Afya Dr Kerry Chant amewakumbusha watu wasitembelee vitongoji vya halmashauri nane isipokuwa kama ni lazima.   

Naye kiongozi wa jimbo hilo Gladys Berejiklian anataka jimbo lake lirekodi chanjo milioni sita kufikia mwisho wa Agosti. Kufikia sasa, idadi ya chanjo milioni 3.9 zimetolewa. 

Pata hapa orodha ya zahanati za chanjo

Queensland

Queensland imerekodi kesi mpya 16 ndani ya jamii, zote ziki ungwa na mlipuko wa sasa.

Afisa Mkuu wa Afya Dr Jeannette Young amewahamasisha wakaaji kutoka maeneo ya halmashauri 11 wabaki nyumbani na wapimwe punde wanapo hisi dalili zozote.

Naibu Kamishna wa Polisi Steve Gollschewski amesema kufikia sasa jeshi la polisi limetoa hati za adhabu 70 pamoja nakuwakamata watu 21, ambao hawaku fuatilia amri za afya ya umma.

Pata hapa kituo cha karibu cha vipimo vya COVID-19. Pata hapa rasilimali zaidi kuhusu coronavirus katika lugha yako.

Hali ilivyo kuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
  • Victoria imerekodi kesi nne mpya ndani ya jamii, zote zikiungwa na milipuko ya sasa na zilikuwa ndani ya karantini wakati zilikuwa katika hali ambukizi.
  • Watu ambao wamepoteza angalau masaa 8 ya kazi kwa sababu amri za afya ya umma jimboni humo, wanastahiki kupokea malipo ya janga ya COVID-19 kwa nyongeza ya malipo yao ya kawaida. Madai ya msaada huo wa ziada yame anza kupokewa leo.

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga

Karantini na masharti ya vipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na mikoa:

NSW Safari & Usafiri na Karantini

VIC Vibali vya safariWasafiri wa ng'ambo na Karantini

ACT Safari na Karantini

NT Safari na Karantini

QLD Safari na Karantini

SA Safari na Karantini

TAS Safari na Karantini

WA Safari na Karantini

Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Pata rasilimali zilizo tafsiriwa na huduma yamawasiliano ya kitengo cha afya cha tamaduni mbali mbali cha NSW hapa:

COVID-19 Vaccination Glossary
Appointment Reminder Tool.


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na mkoa:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania

Northern Territory 


Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo na mkoa:

NSW 

Victoria 

Queensland 

South Australia 

ACT 

Western Australia 

Tasmania
Northern Territory


Share

3 min read

Published

By SBS/ALC Content

Presented by Gode Migerano

Source: SBS




Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps

Listen to our podcasts

Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service

Watch now