Taarifa mpya kuhusu COVID-19: NSW yarekodi siku yapili mfululizo yenye zaidi ya kesi 1,000

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 29 Agosti 2021.

Vaccination clinic at Olympic Park Sydney, NSW

Source: AAP Image/Bianca De March

  • Masharti mapya ya chanjo kwa baadhi ya wafanyakazi wanao idhinishwa jimboni NSW
  • Victoria yathibitisha kuwa muda wa makatazo jimboni humo uta ongezwa
  • ACT yarekodi kesi mpya 13 ndani ya jamii
  • Queensland yarekodi kesi moja ndani ya jamii katika karantini ya nyumbani

New South Wales
NSW imerekodi mesi mpya 1,218 ndani ya jamii, kesi 887 zikiwa katika maeneo ya magharibi na kusini-magharibi Sydney. Watu sita walifariki, nakufanya idadi kamili ya vifo vinavyo husishwa na COVID kufika 145.  

Kuanzia Jumatatu 6 Septemba, wafanyakazi walioidhinishwa wanao ishi katika maeneo ya halmashauri za jiji zenye wasi wasi ila wanafanya kazi nje ya sehemu wanako ishi, wanastahili kuwa na angalau dozi moja ya chanjo ya COVID-19.

Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 92 ndani ya jamii, zikijumuisha kesi mpya 30 ndani ya jamii ambazo hazija ungwa na milipuko ya sasa.

Miongoni mwa kesi 778 zinazo endelea, takriban kesi 500 ziko katika maeneo ya kaskazini na magharibi ya Melbourne, kiongozi wa jimbo hilo Daniel Andrews amesema haitawezekana kumaliza makatazo tarehe 2 Septemba.

Pata vituo vya chanjo karibu yako.

Hali ilivyokuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
  • Queensland itafungua kituo chaku toa chanjo kwa watu wengi, ndani ya Brisbane Entertainment Centre katika eneo la Boondall kuanzia tarehe 8 Septemba.
  • Waziri wa Afya Greg Hunt amesema mpango wakudai chanjo ya COVID-19 utatoa ulinzi kwa wa Australia wanao pokea chanjo ambayo imepewa idhini ya TGA.

Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:

ACT Usafiri na Karantini
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.



Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:

NSW 
ACT 

Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya:

NSW 
ACT 

Share

Published

By SBS/ALC Content
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service