- TGA imependekeza kuwa matumizi ya vipimo nyumbani, yata anza kuanzia 1 Novemba.
- Victoria yarekodi takwimu zajuu zaidi za kila siku, tangu mwanzo wa janga
- Milipuko miwili mipya jimboni Queensland yatambuliwa, siku chache kabla ya fainali ya mchezo wa NRL
Victoria
Victoria imerekodi kesi mpya 867 za COVID-19 ndani ya jamii, pamoja na vifo vingine vinne, hali ambayo imefikisha idadi ya kesi zinazo shughulikiwa kufika 9,261.
Jimbo hilo linazindua jaribio jipya la app, ambayo inaweza tumiwa kuwafuatilia wakaaji wa Victoria wanao rejea jimboni humo kutoka majimbo mengine na ng'ambo.
Queensland
Sehemu mbili za milipuko ya COVID-19 zimetambuliwa mjini Brisbane siku chache, kabla ya fainali ya mchezo wa NRL, ikijumuisha moja inayo mhusu dereva wa lori, ambaye alikuwa katika hali ambukizi kwa muda wa siku nane ndani ya jamii.
Jimbo hilo limerekodi kesi mpya nne ndani ya jamii. Uvaaji wa barakao itakuwa lazima tena kwa wakaaji wa halmshauri za jiji za Brisbane na Moreton Bay.
Bonyeza hapa kupata miadi ya chanjo yako
New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 863 ndani ya jamii za COVID-19 na vifo saba, kesi nyingi zikiwa katika eneo la wilaya ya afya ya Kusini Magharibi Sydney na Magharibi Sydney.
Mamlaka wanazingatia kuweka wakaazi katika halmashauri za jiji za Port Macquarie na Muswellbrook, chini ya amri yakuto toka na, kuongeza muda wa amri yakuto toka katika eneo la Kempsey, kwa sababu ya ongezeko ya kesi katika maeneo hayo.
Australian Capital Territory
Kiongozi wa ACT Andrew Barr amesema njia ya wilaya hiyo kuondoka katika amri yakuto toka nje, ita kuwa kwa kasi ya pole pole, wakati kesi 13 zimerekodiwa. Watu nane wame lazwa hospitalini na virusi hivyo, watatu kati yao waki pumua kwa msaada wa mashine ndani ya kitengo cha matibabu ya hali mahtuti.
Bonyeza hapa ku kuomba miadi yako ya chanjo ya COVID-19.
Hali ilivyo kuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
- Utawala wa Bidhaa za Tiba (TGA) ime pendekeza kuwa, vipimo vya nyumbani vita patikana kuanzia 1 Novemba.
Karantini, safari, zahanati za vipimo na malipo ya janga
Karantini na masharti yavipimo husimamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na wilaya:
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza omba kibali mtandaoni. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari zakimataifa ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali, nakuchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.
- Pata hapa habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60 sbs.com.au/coronavirus
- Pata hapa miongozo inayo faa kwa jimbo au wilaya yako: NSW, Victoria, Queensland, Western Australia, South Australia, Northern Territory, ACT, Tasmania.
- Pata hapa taarifa kuhusu chanjo ya COVID-19 katika lugha yako.
Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa za huduma yamawasiliano ya shirika la afya ya tamaduni nyingi ya NSW:
Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya:
Taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo la wilaya: