Taarifa mpya ya UVIKO-19: Wauguzi waandamana NSW na miadi ya chanjo ya Novavax yapatikana

Hii ni taarifa yako mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa Februari 15.

Nurses hold placards during a nurses’ strike outside the NSW Parliament House in Sydney, Tuesday, February 15, 2022

Nurses protesting against understaffing and difficult work conditions outside NSW Parliament House in Sydney on 15 February 2022. Source: AAP Image/Bianca De Marchi

  • Jimboni New South Wales, wauguzi wana andamana kuomba ongezeko la wafanyakazi wakuwahudumia wagonjwa, pamoja na nyongeza kwa mishahara yao. Hatua hiyo ili anza saa moja asubuhi na itadumu kwa muda wa msaa 24.
  • Maandamano hayo yanafanyika mjini Sydney, mbele ya bunge la NSW.
  • Waziri wa Afya wa NSW alisema uamuzi wa chama cha wafanyakazi kuendelea mbele na maandamano hayo, ni "tendo lakusikitisha", baada ya Tume ya maswala yakazi kuamuru maandamano hayo yasifanywe.
  • Wakati wa maandamano hayo, huduma zakuokoa maisha, zitaendelea katika hospitali zote za umma pamoja nakatika huduma za afya.
  • Chanjo ya Novavax inayo tengezwa kupitia proteini, kwa sasa imo ndani ya zahanati zama GP, maduka yamadawa na katika vituo vya chanjo vinavyo simamiwa na serikali ya jimbo.
  • Chanjo hiyo ime idhinishwa kwa matumizi katika watu wenye zaidi ya miaka 18 kwa dozi zao za kwanza naza pili. Chanjo hiyo kwa sasa haitolewi kwa watu wenye chini ya miaka 18 pamoja na kama chanjo za jeki.
  • Waziri wa Afya wa Shirikisho Greg Hunt anatumai chanjo hiyo itatoa "chaguzi mpya" kwa wale ambao "wame subiri au hawakuweza chukua chanjo zingine zilizo kuwepo.".
  • Tovuti ya Vaccine Clinic Finder kwa sasa inatoa fursa zakutafuta upatikanaji wa chanjo ya Novavax kote nchini Australia.
  • Kiongozi wa Upinzani wa Victoria Matthew Guy ametozwa faini ya $100, kwa kutovaa barakoa ndani ya bunge la jimbo hilo. Wabunge wengine wanne wa Victoria nao pia wame pewa faini.
  • Idadi ya wagonjwa wa UVIKO-19 walio lazwa katika hospitali za Victoria, ni ndogo zaidi tangu mwanzo wa mwaka.
  • Jeshi la Ulinzi la Australia lita saidia kutoa huduma ndani ya vifaa vitatu vya huduma yawazee jimboni Tasmania, ambavyo vime kumbwa na mlipuko wa UVIKO-19, Naibu Kiongozi wa jimbo hilo na Waziri wa Afya Jeremy Rockliff amesema.

Takwimu za UVIKO-19

Jimbo la New South Wales liliripoti idadi ya wagonjwa 1,583 walio lazwa hospitalini, 96 kati yao wakiwa ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti. Kume ripotiwa pia vifo 16, pamoja na kesi mpya za maambukizi 8,201 za UVIKO-19.

Jimboni Victoria, watu 441 wame lazwa hospitalini, 67 kati yao wakiwa ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti na 14 wanapumua kwa msaada wa mashine. Kuliripotiwa vifo 20 pamoja na maambukizi mapya 8,162 ya virusi.

Jimboni Queensland, kulikuwa kesi mpya 5,286 za UVIKO-19 pamoja na vifo 10. Wagonjwa 462 wame lazwa hospitalini, 35 kati yao wakiwa katika kitengo cha wagonjwa mahtuti na 16 kati yao wanapumua kwa msaada wa mashine.

Jimbo la Tasmania halijarekodi vifo vyoyvote, ila kuna kesi mpya 513 za UVIKO-19. Watu 10 wamelazwa hospitalini wakitibiwa UVIKO-19, na mmoja wao yumo ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti.

Na katika jimbo la Kusini Australia kuna kesi mpya 1,138 za UVIKO-19 ambazo zimeripotiwa, watu 219 wame lazwa hospitalini, 18 kati yao wana hudumiwa ndani ya kitengo cha wagonjwa mahtuti na 5 kati yao wanapumua kwa msaada wa mashine.

Kwa hatua zilizopo kwa sasa katika jibu la janga la UVIKO-19 katika lugha yako, bonyeza hapa.


Majimbo kadhaa yana fomu zaku sajili matokeo ya vipimo vya RAT.

Karantini na vizuizi jimbo kwa jimbo

Safari

Msaada wakifedha

Kuna mageuzi kwa malipo ya janga ya UVIKO-19, punde majimbo yanapo fikia viwango vya 70% na 80%  ya watu ambao wame pata chanjo kamili: Kupata msaada wakati wa UVIKO-19 kutoka Services Australia katika lugha yako


 


 



Tazama rasilimali zilizo tafsiriwa nakuchapishwa na shirika la NSW Multicultural Health Communication Service


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na wilaya

NSW 
ACT 

Share

Published

Updated

Presented by Gode Migerano

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service