- Watu 180 wanao husishwa na shule moja Canberra, wamelazimishwa kujitenga kwa sababu ya hofu kuhusu kuwa hatarini kuambukizwa virusi vya Omicron.
- NSW imerekodi kesi sita mpya za Omicron, hali ambayo imepelekea idadi ya maambukizi ya aina hiyo mpya ya kirusi kufika 31.
- Kuanzia 17 December, watu ambao hawaja chanjwa watapigwa marufuku kutoka sehemu zisizo mhimu zakibiashara jimboni Queensland.
- Waziri wa afya wa Queensland ametoa taarifa kuwa, kesi chanya iliyo tambuliwa mjini Gold Coast inaungwa na kituo cha huduma ya wazee ila, kwa sasa hakuna mtu mwingine ndani ya makazi hayo ambaye amepatwa na maambukizi hayo.
- Uchunguzi kutoka shirika la Australian Red Cross umepata kuwa mtu mmoja kati ya watu watatu, hawatazamii msimu wa sherehe waki ulinganisha na miaka ya nyuma na 61%, wana wasiwasi kuhusu jamaa wao ambao wako katika hali mbaya na rafiki zao ambao wana upweke, iwapo vizuizi vya usafiri vita salia.
TAKWIMU ZA UVIKO-19:
Victoria imerekodi kesi mpya 1,185 ndani ya jamii pamoja na vifo saba.
NSW imerekodi kesi mpya 260 ndani ya jamii pamoja na vifo viwili.
ACT imerekodi kesi mpya tatu, nayo Queensland imerekodi kesi moja.
Karantini na vizuizi jimbo kwa jimbo:
Safari
Msaada wakifedha
Kuna mageuzi kwa malipo ya janga ya UVIKO-19, punde majimbo yatakapo fikia kiwango cha 70% na 80% ya watu ambao wamepata chanjo kamili: Kupata msaada wakati wa UVIKO-19 kutoka kwa Services Australia katika lugha yako
- Pata habari na taarifa katika zaidi ya lugha 60 hapa sbs.com.au/coronavirus
- Pata miongozo inayo faa kwa jimbo na wilaya yako hapa: NSW, Victoria, Queensland, Western Australia, South Australia, Northern Territory, ACT, Tasmania.
- Pata taarifa kuhusu chanjo ya UVIKO-19 katika lugha yako.