Jumanne, Australia iliripoti vifo 37 vya UVIKO-19, ambavyo vilijumuisha vifo 11 jimboni New South Wales, 12 Victoria, 6 Queensland na 6 Kusini Australia, na 2 Tasmania. Magharibi Australia iliripoti pia vifo vitatu vyakihistoria.
Idadi ya watu wanao lazwa hospitalini jimboni Queensland imekuwa ikiongezeka katika miezi iliyopita. 12 Aprili, watu 572 walikuwa hospitalini kulinganisha na watu 247 mwezi uliopita.
Serikali ya Australia itatoa dawa ya pili ya UVIKO-19 ya kunywa ambayo daktari lazima atoe kwa mgonjwa, na itatolewa kupitia mfumo wa faida ya mandawa (PBS) kwa wa Australia ambao wako katika hatari ya juu yakupata aina mbaya ya UVIKO-19 kuanzia 1 Mei 2022.
Wagonjwa wenye kiwango kidogo au wastan cha UVIKO-19 na wako kwenye hatari kubwa yakuwa na magonjwa sugu, wanaweza tumia dawa ya kunywa kama 'Paxlovid'. Dawa hiyo inatarajiwa kupunguza mahitaji yakulazwa hospitalini.
Msemaji wa chama cha Labor wa maswala ya uhamiaji na maswala ya nyumbani Kristina Keneally, amepatwa na UVIKO-19. Atajitenga kwa muda wa siku saba.
Shirika la Afya la Dunia (WHO) limeanza kufuatilia aina mpya ya kirusi cha Omicron. Imeongezea BA.4 na BA.5 kwenye orodha yake ya uchunguzi. WHO tayari inafuatilia BA.1 (aina halisi ya kirusi) na BA.2 (aina ya kirusi ambacho hakiko wazi), na BA.1.1 na BA.3.
Wasiwasi imeongezeka Marekani baada ya zaidi ya maafisi 50 wa serikali kupatwa na UVIKO-19, baada ya kuhudhuria tukio lajioni la mchezo wa Gridiron mjini Washington, DC mapema mwezi huu. Maafisa walio ambukizwa wanajumuisha wanachama wa ofisi za Rais na Naibu Rais.
Soma kuhusu Chanjo za UVIKO-19 katika Kiswahili
Pata zahanati ya kupimia UVIKO-19
ACT New South Wales Northern Territory Queensland
South Australia Tasmania Victoria Western Australia
Sajili matokeo ya kipimo chako cha RAT hapa, kama ni chanya
ACT New South Wales Northern Territory Queensland
South Australia Tasmania Victoria Western Australia
Jua kuhusu unachoweza na kile ambacho hauwezi fanya popote nchini Australia
Kabla uende ng'ambo, tazama masharti mapya ya usafiri na ushauri
Kama unahitaji msaada wa fedha, tazama chaguzi zako ni gani
Hapa kuna msaada waku saidia kuelewa maneno yakiufundi ya UVIKO-19 katika Kiswahili
Soma taarifa zote kuhusu UVIKO-19 katika Kiswahili kwenye tovuti ya SBS kuhusu Coronavirus.

